Monday, 5 December 2016

KIFO CHA PROF. IDRISSA MTULIA - MAKALA NA PICHA HISANI YA SALUM MATIMBWA

Prof. Idrissa Mtulia

Marehemu Mzee wetu Prof.Mtulia jana aliswali swala ya Inshaa ktk msikiti wa Shaadhly kama kawaida yake.

Pia alihudhuria shughuli ya kifamilia pale nyumbani kwake akiwa pamoja na ndugu na jamaa. 

Alfajr ameswali kama kawaida na leo ni siku ya Jumataatu kawaida hufunga sunna na leo ameamka na swaum yake ya sunna hii muhimu.

Kawaida huwa anakwenda kazini kwake hospitali ya Tumaini mnamo saa nne asubuhi.

Na leo ameazimia hivyo na wagonjwa wake walikuwa tayari wapo hospitali kusubiri huduma yake.

Akajisikia vibaya kidogo hivyo akaamua kujipumzisha ili ikifika saa ya kwenda hospitali huenda uchovu aliousikia utakuwa umepungua kama si kumtoka kabisa.

MASKINI KUMBE MUDA WAKE WA UHAI NDIO ULIKUWA UMEEISHA,
ALIPOLALA HAKUAMKA TENA.

Vijana wake walipoona muda unaeenda nae hajaoka!! Wakajaribu kumuamsha lakini wapi!! Mja huyu alisharejea kwa muumba wake.

INNA LILAH WAINNA ILLAH RAJUUN


No comments: