Friday, 17 February 2017

KUTOKA JF:MJADALA WA NANSIO KUHUSU UHURU WA TANGANYIKA 1953


Discussion in 'Jukwaa la Historia' started by Mohamed SaidJan 4, 2017.
  1. M

    Mohamed SaidVerified User 

    #1
    Jan 4, 2017
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,487
     
    Likes Received: 3,485
     
    Trophy Points: 280


    [​IMG]

    Wednesday, 4 January 2017

    Aziz Ali
    Kleist Sykes alikuwa na duka la vyakula Kipata Street sasa mtaa huo umepewa jina lake unaitwa Mtaa wa Kleist. Hizi zilikuwa juhudi za Kitwana Selemani Kondo alipokuwa Meya wa Dar es Salaam kuwaadhimisha watu maarufu wa waliopata kuishi Dar es Salaam na wakaitumikia jamii. Nilipata kumsikia Mzee Kondo akisema, ‘’Hivi vipi litawekwa jina la mtu ambae hana nasaba yoyote na mji wa Dar es Salaam katika mji huu na kuwaacha wenye mji wao?’’ Hakika jambo hilo halikughalis. Mzee Kondo aliendelea na kusema, ‘’Hivi jina la Matola kwa nini lisiwekwe Dodoma lije liwekwe Dar es Salaam na wakati huo huo wakawasahau wazee wetu wa Dar es Salaam?

    Turejee kwa Kleist Sykes. Hili duka lilikuwa nyumbani kwake na hapo ndipo ilipokuwa barza ya wazee maarufu wa mjini kukutana jioni inapoingia alasiri kuzungumza. Miaka ile Dar es Salaam kulikuwa na wauza kahawa wanapita mitaani na kahawa zao ndani ya madeli ya shaba yanayong’aa kwa kupigwa braso wakiuza kahawa na wao wenyewe wamevaa nadhifu, kikoi na kizubau na kofia kichwani. Basi baraza ile kila muuza kahawa akipita ataitwa na kuagizwa apige duru kwa wanabarza. Ikawa pale ile barza waungwana wale wanakunywa vikombe na vikombe vya kahawa hadi wanapoagana Maghrib inapoingia.

    Mmoja wa wanabarza wa barza hii alikuwa babu yangu Salum Abdallah ambae nyumba aliyokuwa anaishi ilikuwa inatazamana na nyumba ya Kleist. Hawa walikuwa si majirani tu bali hata kazi wanafanya pamoja Tanganyika Railways. Hii ilikuwa miaka ya mwanzo ya 1920. Kleist akiwa Karani wa Mahesabu na babu yangu Mfua Vyuma kwenye karakana ya Railway iliyokuwa Arab Street sasa Mtaa wa Nkrumah. Mle ndani kulikuwa na king’ora kikipigwa saa moja kamili asubuhi barabara na saa saba mchana. King’ora hiki cha Railway kiliwasaidia sana wakazi wa Kariakoo na Ilala kujua majira.

    Mtu mwingine maarufu katika ile barza alikuwa Aziz Ali, Mdigo kutoka Moa Tanga. Huyu Aziz Ali alikuwa mwamba katika miamba ya Dar es Salaam. Alikuwa tajiri ‘’contractor,’’ wa kujenga, majumba, Mwafrika wa kwanza kununua gari na kujenga nyumba ya vigae na vioo Mtoni. Nyumba hii hadi leo ipo na sehemu hiyo katika Kilwa Road inaitwa Mtoni kwa Aziz Ali. Lakini katika sifa hizi sifa yake kubwa sana Aziz Ali ilikuwa ujenzi wa misikiti na kuihudumia misikiti. Hii ilikuwa miaka ya 1930 na hapakuwa na umeme Kariakoo. Misikiti ilikuwa ikitumia karabai kuonea. Aziz Ali yeye alinunua karabai kwa kila msikiti na ikifika Maghrib mwanae Hamza alikuwa akizitia mafuta na kuziwasha kisha akizipeleka kila msikiti tayari kwa sala ya Maghrib. Inapomalizika sala ya Isha alikuwa anapita tena katika ile misikiti kukusanya karabai zake na kurudi nazo nyumbani kwao Mtaa wa Mbaruku na Kongo. Hii ndiyo ilikuwa kazi yake kila siku. Aziz Ali alipokufa mwaka wa 1951 miaka miwili baada ya kifo cha rafiki yake Kleist gazeti la Tanganyika Standard liliandika kifo chake kwa maneno haya: ‘’Aziz Ali the Builder of Mosques is Dead,’’ yaani, ‘’Aziz Ali Mjenzi wa Misikiti Amekufa.’’ Iko siku nilimtembela Rose Aziz mjukuu wa Aziz Ali, mtoto wa Hamza Aziz. Rose akanionyesha picha katika ukumbi wake ya mtu amevaa tarabushi akanambia, ‘’Mohamed unamuona mume wangu?’’ Nikiwa katika hali ya kushangaa huku nikiikodolea macho ile picha Rose akaendelea, ‘’Huyu babu yangu Aziz Ali.’’

    Aziz Ali alikuwa na nyumba nyingi sana Dar es Salaam na ndiyo zilikuwa moja ya utajiri wake. Katika nyumba hizi nyumba ambayo imaecha historia ya pekee ni hii nyumba ya Mtaa wa Mbaruku na Congo kwa sababu nyumba hii ilikuwa moja ya sehemu ambazo harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika zilianza. Nyumba nyingine ilikuwa Mtaa wa Kipata kwa Ally Sykes, hapo zamani lilipokuwa duka la baba yake na barza ya wazee. Nyumba nyingine ilikuwa Stanley Street kwa Abdul Sykes. Nyumba hii ilikuwa pia ya Kleist na kulikuwa na duka la vifaa vya ujenzi katika uhai wake. Hii ilikuwa mwanzoni mwa mwaka wa 1950. Mambo yalipamba moto sana kuanzia mwaka huo pale vijana wazalendo walipoanza kufanya mipango ya kuunda chama cha siasa halisi kupambana na ukoloni wa Muingereza. Hizi ndizo zikawa nyumba ambazo Nyerere alikuwa akifika kuanzia mwaka wa 1952 kila anapokuja mjini kutokea Pugu alipokuwa akifundisha. Mama Ali mke wa Aziz Ali bado yu hai, Bi Mkubwa huyu ana mengi katika historia ya nyumba ile ya Mbaruku alipokuwa akiishi na mumewe katika miaka ile ya 1940 na akaendelea kuishi hapo na wanawe baada ya kifo cha mumewe. Hivi sasa Mama Ali anaishi Ilala na ni mtu mzima sana.

    Angalia picha:Mohamed Said: AZIZ ALI WA GEREZANI NA MTONI DAR ES SALAAM
  2. babumapunda

    babumapundaJF-Expert Member

    #381
    Yesterday at 12:28 PM
    Joined: Dec 21, 2012
    Messages: 3,474
     
    Likes Received: 1,357
     
    Trophy Points: 280




    upo vizuri




  3. M

    Mohamed SaidVerified User 

    #382
    Yesterday at 2:34 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,487
     
    Likes Received: 3,485
     
    Trophy Points: 280




    Mtanganyika...
    Utakumbuka nilikuambia kuwa kuna mtu aliniomba ruksa akutukane nami
    nikamkataza.

    Baada ya wewe kurejea tena hapa Majlis na matusi mara ya pili na mie kukupa
    jibu hilo hapo juu karejea tena na ombi lile lile...

    Nimemkatalia lakini nimemuahidi kukuandika na kukupa maelezo lao kwa ufupi
    kuhusu Hamza Mwapachu.

    Ikiwa umefuatilia darsa langu kuhusu tatizo lililotokea katika kuandika historia ya
    TANU ndani ya wana TANU wenyewe akiwemo Abdul Sykes, Julius Nyerere,
    Saadan Abdu Kandoro 
    na Mwalimu Kihere utaona kuwa ilifika mahali Abdul
    Sykes 
    jina lake liliondolewa kabisa katika historia ya TANU na likawa halitajwi wala
    kuhusishwa na siasa za kupigania uhuru wa Tanganyika.

    Ikawa hata ilipoandikwa historia ya TANU na Kivukoni College mwaka wa 1981
    haikuelezwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA 1953 kutoka kwa nani.

    Lakini mimi nilipoandika kitabu cha Sykes nilieleza kwa kirefu uchaguzi wa 1953
    wa urais wa TAA kati ya Abdul Sykes na Nyerere uliofanyika Ukumbi wa Arnautoglo
    tarehe 17 April, uchaguzi ambao ndiyo ilikuwa ngazi ya Nyerere ya kwanza kupanda
    na kuwa kiongozi wa watu wa Tanganyika.

    Katika kitabu cha Sykes nimeeleza vipi Nyerere alishinda uchaguzi ule dhidi ya Abdul.

    Kitu ambacho sikueleza na sababu ni kuwa ilikuwa sikijui ni mazungumzo aloyofanya
    Abdul Sykes na Hamza Mwapachu Nansio, Ukerewe ambako Hamza alikuwa anafanya
    kazi.

    Agenda ya mazungumzo yale ilikuwa Nyerere.

    Katika mazungumzo haya alikuwapo pia Ali Mwinyi Tambwe aliyekuwa Katibu wa Al
    Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

    Abdul alikwenda kwa Hamza kutaka ushauri na neno lake la mwisho kuhusu Nyerere
    kuachiwa kiti cha rais wa TAA na Abdul 1953 na mwaka unaofuatia waunde TANU.

    Hamza alimwambia Abdul kuwa yeye hajabadili mawazo na alimtaka Abdul amsaidie
    Nyerere kushinda uchaguzi ule.

    (Habari hizi kaziandika Juma Mwapachu miaka ya hivi karibuni baada ya kusoma makala
    yangu moja).

    Juma Mwapachu akihojiwa katika uzinduzi wa kitabu cha Mwalimu Nyerere,''The Early Years,'' kilichoandikwa na Thomas Morlony


    Hivi ndivyo Nyerere alivyokuja kuingia katika uongozi wa TAA 1953 na viongozi wake
    ni hawa hapo chini:

    J. K. Nyerere, Rais, Abdulwahid Sykes, Makamu wa Rais; J. P. Kasella Bantu, Katibu
    Mkuu; Alexander M. Tobias na Waziri Dossa Aziz, Katibu wa pamoja wa muhtasari;
    Wajumbe wa kamati: Dr Michael Lugazia, Hamisi Diwani, Tewa Said Tewa, Denis
    Phombeah, Z. James, Dome Okochi,
     C. Ongalo na Patrick Aoko.

    Katika historia hii ndipo unapokuja umuhimu wa Hamza Mwapachu na Abdul Sykes
    katika historia ya uhuru wa Tanganyika na maisha ya Nyerere.

    Mtanganyika...
    Nakuhitimishia kwa kukueleza kuwa moja ya sababu kubwa ya Hamza kutaka Nyerere
    achukue uongozi ni kuwa alimwambia Abdul kuwa Waingereza hawatakuwa na hofu
    kujadili uhuru wa Tanganyika na Nyerere kwa kuwa ni Mkristo.

    Mimi nimemjua Juma Mwapachu toka 1967 angalia picha tuliyopiga pamoja miaka hiyo
    wa kwanza kulia ni Mwandishi, William Mfuko, Juma Mwapachu, Andrew Gordon,
    Edward Makwaia 
    (sasa mmoja wa machifu Usukuma), Huyo Bi. Mkubwa ni mama yake
    Edward, Mama Mary Mackeja na nyuma yake ni Wendo Mwapachu:

    [​IMG]
  4. M

    Mohamed SaidVerified User 

    #383
    Yesterday at 9:38 PM
    Joined: Nov 2, 2008
    Messages: 9,487
     
    Likes Received: 3,485
     
    Trophy Points: 280




  5. Zakumi

    ZakumiJF-Expert Member

    #384
    Today at 7:01 AM
    Joined: Sep 24, 2008
    Messages: 4,673
     
    Likes Received: 66
     
    Trophy Points: 145
    New




    Mkuu unayo ruhusa ya kutukana watu, lakini tutajie kwenu wapi na mchango wa watu wa kwenu kwenye uhuru wa Tanganyika.

No comments: