SALAMU KUTOKA KWA MASHEIKH WALIOKO MAHABUSU KATIKA GEREZA LA
SEGEREA
Jumamosi hii ya tarehe 11 Februari 2017 kundi la vijana walio
katika kundi la Udugu wa Kiislamu walifanya ziara katika Gereza la Segerea kwa
lengo la kuwapelekea masheikh zawadi na kuwajulia hali.
Pamoja na yote.
Kwanza masheikh wanawasalimu Waislamu wote na
wameomba Waislamu wasiwasahau kwa dua.
Pili wamesema kuna wimbi kubwa la watu kusilimu ndani ya
gereza, na kubwa zaidi wamepata wachungaji wawili walioingia katika haki.
Kwa ajili hii basi kwa sasa wanakabiliwa na uhaba wa nguo (kanzu
na misuli) kwa ajili ya kuswalia hasa kutokana na nguo chache walizokuwa nazo
kuwapa ndugu zao wanaoingia katika Uislam.
Wanawaomba Waislamu kwa umoja wao kuwapelekea nguo hasa kanzu na
misuli ili waendelee kudumisha ibada kwa wepesi na wawafariji wale wanaoingia
katika Uislam kwa wingi sana.
Tunaomba mwenye kuwa na nafasi ya kupata hivi vifaa wawasiliane
na Amiir Qudrah simu no. 0715580807 au 0625768718.
No comments:
Post a Comment