Utangulizi
Nilipokuwa nasoma hizo beti za Kibatari nimepata faraja kuona kuwa Wazanzibari wamejifunza kujicheka na hii ni ishara nzuri. Huku kunashusha shinikizo la damu na huleta kicheko moyoni na kicheko huleta nuru katika uso. Nuru nayo huangaza pote.
Kibatari |
Ewe wangu kibatari
Utulize moyo wako
Wewe bado u mzuri
Liondowe sononeko
Umeme ulinighuri
Kukusahau mwenzako
Lakini sasa tayari
Takutafuta uliko
Na mie takugomeya
Nitoe kiburi chako
Wa Zeco ushazoweya
Huo ndo kiasi chako
Sasa kaka subiriya
TANESCO kiboko yako
Kibatari kibatari
Sikama sijakikubali
Kimelea wasomi mahiri
Hata huwezi amini
Swali langu jamani
Naomba mnijibuni
Wenye kosa ati ni walipaji kwani?
Suali hili ni kubwa
Liende mbele sambamba
Siku, wiki Na mwezimbamba
Mifuko yetu mwairamba
Tuelezwe kwa makini Kosa hili ni la
naniiii?
Mbona mwababaisha sana huku mkifunga
goli porini
Kibatari nakupenda Ila utaua
jamaniiiii
Ndugu yenu kibatari
Sitaki chenu kiburi
Mlinitupa duhuri
Kwa hiyo yenu ghururi
Na nyingi zenu shururi
Niliweza zisubiri
Nikawa kama kaburi
Wala hamnidhukuri
Mlikuwa mwafikiri
Kuwa mimi ni faqiri
Wapi wenu uhodari
Na ule ujemedari
Nawapeni tahadhari
Kosa msilikariri
Munitundike vizuri
Kwenye uzi wa hariri
No comments:
Post a Comment