Sunday, 12 March 2017

KUTOKA JF: AUDIO NA VIDEO ZA MOHAMED SAID


Patriot

Huwa nami wakati mwingine naona shida kujieleza hivyo lakini ndiyo 
lazima nizitoe hizi taarifa vinginevyo lengo la kusomesha historia hii 
halitafikiwa.

Waamerika wamelitafutia dawa tatizo hili huwa wana kitu wanaita, 
"bragging," hapo unapewa uwanja wa kujieleza kwa kutamba bila 
hofu ya kuonekana una upungufu wa ustaarabu. 

Wamefanya hivi kuondoa tatizo hili ulioliona wewe ambalo nami huwa 
linanisumbua.
Mohamed Said said: 
Pukudu,
Makala zangu nyingi na mada nilizoandika na kuwasilisha katika vyuo mbali
mbali utazipata katika www.mohammedsaid.com.

Nimeandika vitabu kadhaa na kufanya mahojiano na vyombo vingi vya habari
ndani na nje ya nchi kuhusu historia hii.

Unaweza kusikiliza audio na kuangalia video katika hiyo blog yangu.

Unaweza pia kuzipata baadhi ya DVD zangu katika maduka mengi khasa mjini
Dar es Salaam na katika miji mikubwa nchini.

Nasema Amin kwa dua yako.

[​IMG]

Hii ''cover,'' ya DVD kanirushia mpwa wangu juzi Ijumaa alikwenda kuswali Msikiti wa
Mtambani akakuta inauzwa hapo nje.

Mpwa wangu akanitania katika ujumbe alionitumia akasema, ''Mjomba sikuwa najua
kuwa wewe ni Ph D...''

Uzuri wake ni kuwa mimi hata sijui ni nani anatengeneza hizi DVD na kuziuza.

No comments: