Paul Sozigwa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere
Leo
asubuhi mapema kabisa rafiki yangu mmoja wa Kariakoo kanifikishia taarifa katika
‘’whatsapp,’’ kuhusu msiba uliotufika wa Mzee Paul Sozigwa. Nami nikasita
kusamabaza kwa kuhofu isije habari si za kweli maana umezuka mtindo wa maskhara
ya kijinga. Si kama simwamini mpashaji wangu la hasha, ila wakati mwingine inapendeza
kwa mtu kuchukua tahadhari.
Mzee
Sozigwa ni jirani yangu nyumba kwa nyumba na wanangu wangu wanamwita babu na
mkewe bibi. Kwa ajili hii basi nikifahamu ugonjwa wa Mzee Sozigwa na kulazwa
kwake hospitali. Lakini kubwa zaidi ni kuwa mke wangu na binti ya Mzee Sozigwa, Salome walikuwa mashoga
wakati wanasoma pamoja shule ya Kisutu Girls kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne kisha Korogwe Girls kidato cha tano hadi cha sita na baadae Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Kwa ushoga huu wao basi mkewe Mzee
Sozigwa kwetu sisi ni mama yetu.
Haraka
sana baada ya kuthibitisha msiba nikampelekea taarifa ya msiba huu rafiki yangu
ambae sitamtaja jina kwa kuwa sijamuomba ruhusa ya kutumia aliyoandikia kuhusu
Mzee Sozigwa kwa hofu ya kunikatalia na hivyo kupoteza historia muhimu katika
nchi yetu kwani hatoandika tena haya aliyoaniandikia.
Yeye
Mzee Sozigwa alikuwa rafiki yake wa karibu sana katika miaka ya mwishoni 1970
wakikutana katika mapenzi ya club ya mpira ya Pan Africa ya Dar es Salaam. Siku
zile tukikaa akinihadithia mengi katika ‘’massive intellect,’’ ya Mzee Sozigwa.
Lakini
raha yenyewe iko hapa. Huyu sahib yangu Mashaallah ana kichwa si cha kawaida.
Nitaweka hapa aliyoniandikia kuhusu Mzee Sozigwa nanyi mpate kufaidi. Sahib
yangu anasema hayo hapo chini kuhusu Mzee Sozigwa:
‘’Nilipata
kuwakaribu sana na Mzee Sozigwa na tukaelewana na kupatana sana zile enzi za
mpira Pan African. Mimi tukaelewana sana katika siasa za mitaani zilizoingia katika
vilabu vya Yanga na Simba. Tukijadili sana tukiwa na marehemu Sam Mdee.
Nikagundua huyu ni mkali sana kichwani!
Jumapili moja tuliangusha mjadala juu ya makala ikitoka katika Sunday
News kila wiki katika miaka ya 1970. Ilikuwa ikiandikwa kutoka Uingereza. Ikiwa
na, ‘’heading.’’ "What they Say about Us." Mdee alikwama katika ‘’analysis,’’
ya nini kilichojificha, ‘’between the lines,’’ ya ile makala ambayo siku ile
ilikuwa ikionesha kumsifu Mwalimu. Nyerere. Mdee aliona sifa. Mzee Sozigwa
hakuona hivyo. Mie nikawa mtu wa kuduwaa, tu. Wakati huo Mdee Mwandishi na Msaidizi
wa Mwalimu Nyerere Ikulu.’’
Naomba
tusimame hapa nieleze machache ya makala haya kwani rafiki yangu hakueleza
muktadha yake lakini mimi na yeye tulipata mara kadhaa kuijadili na akanipa
michapo ya Mzee Sozigwa jinsi alivyotembea katikati ya mistari ya huyu
mwandishi Muingereza.
Kilichotokea
ni kuwa huyu Mwingereza alikwenda kufanya mahojiano na Mwalimu Nyerere nyumbani
kwa Mwalimu Msasani. Sasa aliporudi kwao akaandika makala na katika makala hayo
kwanza, akaanza kwa kumsifia Nyerere na ‘’simplicity,’’ yake akasema watumishi
waliokuja kuwaletea vinywaji walikuwa hawakuvaa nguo nadhifu hivyo na
ukiangalia kama vile hazikupigwa hata pasi. Akaendela na kusema na ‘’juice,’’
aliyopewa ilikuwa ya moto haikuwa baridi akigongea labda nyumbani kwa Mwalimu
hakuna jokofu kiasi inabidi wageni wake wanywe vinywaji vya moto.
Lakini
jinsi alivyokuwa akieleza anakupa picha kuwa anamsifia Mwalimu kwa kutopenda
makuu tofauti na viongozi wenzake wa Afrika mfano wa Mobutu waliokuwa wakiishi
katika maksri.’’ Makala yale yalikuwa yanapita katika hali kama hii. Ni miaka
mingi sana imepita siwezi kukumbuka kila kitu. Makala hii na mfano wa hizi
zikawa zinachapwa na Daily News chini ya ‘’What They Say About Us,’’ wakati ule
mhariri alikuwa Frene Ginwalla mama aliyekuwa akiwajua vyema Waingereza na
vitimbi vyao na kejeli zao.
Sasa
Mzee Sozigwa akawa anamwambia Sam Mdee, ‘’Huyu Mzungu hasifii huyu, huyu
anaponda. Msomeni vizuri mtaona.’’ Lakini kama alivyoeleza sahib yangu, Sam
Mdee yeye aliona Mwalimu kasifiwa kwa kutopenda makuu. Enzi zile zilikuwa enzi
za siasa ya Ujamaa. Mzee Sozigwa yeye kaona Mzungu alikuwa anamdhihaki Mwalimu
Nyerere na alikuwa na sababu nzito za kukubalika.
Huyu
ndiye Mzee Sozigwa. Bingwa wa vijembe na kucheza na maneno, pia mtu wa kusikia
yale ambayo hayakutamkwa, mpita katikati ya mistari ya waandishi. Hakuishia hapo
tu. Paul Sozigwa akikaa nyuma ya ‘’microphone,’’ katika studio anasoma
alichokiandika mwenyewe utasema yuko kakaa katika jamvi anazungumza na wewe na
wala haitakujia fikra kuwa anasoma utadhani anasema.
‘’Topic,’’
yoyote atakayoizungumza katika radio wewe utamsikiliza hata kama hutaki. Huwezi
kubadilisha stesheni wakati Mzee Sozigwa yuko hewani. Huo ni muhali mkubwa.
Sasa
hebu turudi tena kwa rafiki yangu tumsikilize anavyosema kuhusu rafiki yake Mzee
Sozigwa:
‘’Sozigwa
Mkurugenzi TBC. Sozigwa akipenda kunibishia kila nilipokuwa na hoja ya kutoa ‘’Public
Statement,’’ redioni kuhusu, ‘’controversies,’’ baina ya club na, ‘’other
authorities.’’ Kumbe sababu yake kubwa ilikuwa kuni "shape" katika, ‘’thinking
approaches,’’ zangu na hoja zake.
Alifika mahali akawa na, ‘’great confidence,’’ kwangu na akizipenda hoja
nilizozijenga; kiasi kwamba siku moja nilikuwa na, ‘’statement,’’ nzito na
nyeti.
Tulianza
kubishana ofisini kwake TBC. Aliporidhika akatoa amri nii ‘’record,’’ yote na
itolewe hivyo katika kipindi cha michezo. Na ili kuhakikisha inatoka vizuri,
aliamrisha mtu wa zamu aende kunirekodi katika, studio za ‘’External Services,’’
kulikokuwa na vifaa vya kisasa. Akaniweka jikoni studio, na ‘’recorder,’’ akawa,
‘’next room,’’ tunaenda kwa, ‘’signal lights.’’
Mimi
binafsi namkumbuka Mzee Sozigwa katika mkutano wa viongozi wa Jumuia ya Madola Singapore
na TBC wakawa wanamrusha Paul Sozigwa mubashara kutoka Singapore mara baada ya
taarifa ya habari ya saa mbili usiku. Utafurahi na nafsi yako. Paul Sozigwa
mwenyewe hatajitambulisha kama ‘’Paul,’’ bali, ‘’Paulo,’’na ‘’Singapore,’'
ataitaja kama, ‘’Singapura,’’ na si bure anafanya hivi, hicho ni moja ya
vijembe vyake kwa Waingereza kulibadili jina lake likae Kiswahili. Paul Sozigwa
ataeleza yaliyopitika katika mkutano kisha atachomeka kijembe kidogo. Wakiwa Singapore
iko siku ilikuwa ya mapumziko hakuna kikao. Ungetegemea siku hiyo pasiwe na
kipindi mubashara cha Paul Sozigwa kutoka, ‘’Singapura,’’ hata kidogo, Paul
Sozigwa akaingia katika kueleza viongozi waliojimwaga kucheza, ‘’golf,’’ ile
siku ya mapumziko na viongozi wenzao katika viwanja.
Ukweli
ilikuwa Paul Sozigwa alikuwa anawananga viongozi wa nchi za Kiafrika kuwa wao
na ‘’golf,’’ wapi na wapi hasa wakati Afrika ya Kusini imekaliwa na Makaburu na
nchi nyingine za Afrika bado ziko mikononi mwa wakoloni. Sasa njoo hapo anapoaga,
‘’signing off,’’ kutoka Singapore yeye ataaga kwa kusema, ‘’Huyu ni Paulo
Sozigwa kutoka Singapura.’’
Iko
siku Mzee Sozigwa alikuja nyumbani kwetu baada ya kutembelewa na Prof. Emmanuel
Bavu kisha akamleta Prof. Bavu kwetu. Prof. Bavu alikuwa mwalimu wetu mimi na mke
wangu Chuo Kikuu Cha Dar es Salaam. Siku zote Mzee Sozigwa tukisalimiana
kijuujuu tu ninapomwona nje ya nyumba yake lakini siku ile nilikuwa karibu na
yeye, kwangu mimi hii ilikuwa heshma kubwa na jambo la kihistoria. Nilimwomba
tupige picha na alinikubalia.
Waandishi
wa leo hasa watangazaji wana mengi ya kujifunza kwa Mzee Sozigwa.
Picha
aliyoniachia Mzee Sozigwa ni kumuona kila Jumapili asubuhi bila kukosa
akifuatana na mkewe kwenda kusali kwenye kanisa lao Kigamboni.
Naamini
wanaomjua vizuri zaidi Mzee Sozigwa watamwandikia taazia stahili yake.
Kulia: Paul Sozigwa, Mwandishi na Prof. Emmanuel Bavu
|
Friday, 12 May 2017
TAAZIA: RAFIKI YA PAUL SOZIGWA ANAMZUNGUMZA MZEE SOZIGWA RAFIKI YAKE WA ZAMANI
About Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment