Thursday 28 September 2017

MNAKASHA BAINA YA PROF. ASARIA C. MBUGHUNI NA MOHAMED SAID KUHUSU HISTORIA YA TANU

Kushoto: Dossa Aziz, Julius Nyerere, Abdulwahid Sykes na Lawi Sijaona

Abulkarim Ally:Yapo malalamiko mengi sana kuhusu harakati za uhuru na wale walioshiriki ipo dhana inayolaumu kuwa Tanu chini ya Mwalimu Nyerere haikufanya juhudi za kutosha kuandika historia ya harakati za kupigania uhuru na dhana hiyo inadai ni kumuweka juu Mwalimu na kuwasahau wengine. Mohamed Said Salum yeye katika maandishi yake ameandika mengi kuhusu walioshiriki harakati hizo lakini bila msaada wa serikali bado historia ya kweli ya harakati za uhuru na walioshiriki itakuwa haijaandikwa kwa ukamilifu na usahihi uliokamilika.

Emmanuel Muganda nadhani Sh. Mohamed Said Salum ameweka bayana kila kitu na sina haja ya kueleza zaidi. Please refer to his chat.

Mohamed Said Tatizo katika historia hii ni kuwa kuna waliokuja kuona kuwa kuundwa kwa TANU was, ''the ultimate prize,'' na huyu ambae atalivaa taji lile jina lake halitosahaulika katika historia ya Tanganyika. Hii ndiyo sababu hata Chuo Cha Kivukoni kilipokuja kuandika historia ya TANU jina la Abdul Sykes likaondolewa. Vipi utaondoa jina la Abdul wakati hiyo mikutano ya siri ya kuunda TANU ikifanyika nyumbani kwake? Mfano mwingine ni kuwa wanachama wote wa mwanzo kama Dossa, Said Chamwenyewe, Idd Faiz Mafungo, Idd Tosiri, Tatu bint Mzee, Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Suleiman Takadir, Mshume Kiyate, Haidar Mwinyimvua kuwataja wachache na hawa wana mengi walifanya katika kujenga chama, hawamo katika kitabu kile.

Kushoto: Idd Faiz Mafungo, Sheikh Mohamed Ramiyya, Julius Nyerere,
Saadan Abdu Kandoro na Haruna Taratibu

Kushoto kwa Mwalimu Julius Nyerere ni Sheikh Suleiman Takadir
Mwaka wa 1988 gazeti la Africa Events (London) lilipochapa makala yangu, "In Praise of Ancestors," gazeti liliondolewa kwenye ''circulation,'' kwa kuwa nilieleza historia ya Abdul Sykes katika kuunda TANU na mchango wa Al Jamiatul Islamiyya katika kutoa viongozi wa mwanzo na wanachama wa TANU.

Ukimleta Abdul katika historia ya TANU  lazima umlete na baba yake na wadogo zake wote kisha lazima umlete Hamza Mwapachu na watu wengine kama Earle Seaton na Chief Kidaha Makwaia na lile jopo la masheikh wakiongozwa na Sheikh Hassan bin Amir na utake usitake lazima urudi nyuma 1929 kwenye historia ya African Association na historia ya Al Jamiatul Islamiyya fi Tanganyika.

Hamza Kibwana Mwapachu

Katika historia hii utasema kuwa hata hilo jengo ilipoundwa TANU hiyo nyumba ilijengwa na baba yake Abdul kati ya 1929 na 1933 na Abdul akiwa mtoto wa miaka 5 baba yake alikuwa kila Jumapili akimchukua pale New Streets kuangalia ujenzi ule.

Mohamed Said Salum Asante! Kuna mengi ya najifunza na mimi nitaendelea na utafiti. Nimeona ripoti nyingi za mikutano ya miaka 1949 mpaka 1954. Kuna mpaka huyu Muafrika Kusini wa Ki-Zulu Thomas Plantan aliyepata matatizo akafungwa jela. Najaribu kuunganisha vitu ninavyosoma kwenye vitabu vilivyochapishwa, pamoja na chako, na primary sources ninazosoma. Mara nyingine nakuta ripoti zinasema vingine, hata za mikutano ya TAA (1951-53). Naelewa kwamba sio kila kitu kiliwekwa kwenye ripoti ni kweli na kwamba kuna vingine havikuwekwa. Hata hivyo yote haya ni njia ya kutafuta "ukweli."

Thomas Plantan

Kwa upande wangu, kuna simulizi nyingi nimepata hata kwa mzee wangu.  Nimehangaika kupata ushahidi wa kuthibitisha baadhi ya vitu alivyoniambia; mengine nimepata, mengine sijapata.  Cha muhimu ni kulimbikiza ushahidi wakati mwandishi anaandika kuhusu kitu.  Hilo nimejifunza graduate school kwenye falsafa ya taaluma ya historia.  Na sio lazima mtu awe mfuasi wa Buddhism kuandika kitabu cha Buddhism; kwa mtazamo huo, ina maana Mutahaba asingeweza kuandika kitabu cha Ali Migeyo. Fani ya historia inatupa hatua tunazoweza kufuata kutafuta nyaraka, kuchambua, na kuandika.  Kwa ujumla ninachosema ni kwamba, baadhi ya vitu nilivyosoma, hoja itakuwa na nguvu zaidi pale kwenye vyanzo vingi (multiple source) vinavyosema kitu kimoja.  Kama chanzo kimoja kinasema hili na vingine vingi vinasema lile, hapo kunakuwa na utata.

Ali Migeyo

Pamoja na watu wengi uliowataja wewe kwamba historia zao hazikuandikwa, kwanini historia za hawa wa miaka ya arobaini, hamsini pia hazijaandikwa.. Stephen Mhando, Kirilo Japhet, Dr. Joseph Mtangarwa, Dr. Kyaruzi, Dr. W.E.K. Mwanjisi, huyu Mzulu mwingine kutoka Afrika Kusini aliyekuja Tanganyika-Henry Muli, Godfrey Kayamba, na wengine?  Hawa nao historia zao zilizimwa?

Prof. Azaria Mbughuni☝🏿anamjibu Mohamed Said

Azaria nami nanufaika sana na fikra zako. Nadhani umemkusudia Schneider Abdillah Plantan mdogo wake Mwalimu Thomas Saudtz Plantan. Schneider yeye ndiye alifungwa Mwanza wakati wa WWII kwa kuwa alikuwa akiwashawishi watu kumuunga mkono Hitler. Schneider alikuwa matata sana. Alipigana na Kleist katika jeshi la Wajerumani katika WWI chini ya Kamanda Von Lettow Vorbeck dhidi ya Waingereza. Schneider ndiye aliyetia nguvu Abdul Sykes na Dr. Kyaruzi waingie katika uongozi wa TAA  1950 na kaka yake Thomas Plantan na Clement Mohamed Mtamila raus na katibu watoke katika uongozi. Baada ya uhuru Schneider akawa katibu wa Daawat Islamiyya chini ya uongozi wa Mufti Sheikh Hassan bin Amir. Nyerere alimweka kizuizini. Alipotoka alimkabili Nyerere nyumbani kwake Msasani  uso kwa macho akamtukana na kumpa changamoto amfanye atakacho. Katika kitabu cha Abdul Sykes nimetaja mchango wa Stephen Mhando na ndugu yake Peter katika TANU. Pia nimeeleza historia ya Dr. Mwanjisi na yupo katika  Nyaraka za Sykes. Sasa hilo swali kama hawa nao historia zao zilizimwa hilo si swali la kupata jibu kutoka kwangu. Mimi nimesoma majalada ya Sykes yenye historia ya zaidi miaka 100 sasa na ina mengi kuhusu historia ya Wajerumani na Waingereza na wazalendo waliokuja kuunda TANU na kupigania uhuru wa Tanganyika. Umemkusudia Dr. Joseph Mutahangarwa na nikufahamishe kuwa mimi ndiye katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza kuwa katika harakati za TAA kulikuwa na madaktari watano: Dr. Joseph Mutahangarwa, Dr. Vedasto Kyaruzi, Dr. Wilbard Mwanjisi, Dr. Michael Lugazia na Dr. Luciano Tsere.

Sheikh Hasan bin Amir na Julius Nyerere

Azaria kuna kitu nataka nikufahamishe kuhusu Japhet Kirilo na Abdul Sykes na nyaraka nimeziona katika majalada ya Sykes. Abdul ndiye aliyemuomba Earle Seaton kutengeneza petition ya Meru Citizen's Union ya akina Kirilo kwenda UNO. Waingereza walimnyima Kirilo pasi ya kusafiria na Abdul alisimama kidete hadi wakoloni wakampa pasi kwenda UNO akifuatana na Seaton. Hii ilikuwa 1952 na 1953 Kirilo akaungana na Saadan Abdu Kandoro na Abbas Sykes kuzunguka Tanganyika kueleza mgogoro wa ardhi ya Wameru.

Mohamed Said Salum Asante! Kuna mengi ya najifunza na mimi nitaendelea na utafiti. Nimeona ripoti nyingi za mikutano ya miaka 1949 mpaka 1954. Kuna mpaka huyu Muafrika Kusini wa Ki-Zulu Thomas Plantan aliyepata matatizo akafungwa jela. Najaribu kuunganisha vitu ninavyosoma kwenye vitabu vilivyochapishwa, pamoja na chako, na primary sources ninazosoma. Mara nyingine nakuta ripoti zinasema vingine, hata za mikutano ya TAA (1951-53). Naelewa kwamba sio kila kitu kiliwekwa kwenye ripoti ni kweli na kwamba kuna vingine havikuwekwa. Hata hivyo yote haya ni njia ya kutafuta "ukweli."

Kwa upande wangu, kuna simulizi nyingi nimepata hata kwa mzee wangu.  Nimehangaika kupata ushahidi wa kuthibitisha baadhi ya vitu alivyoniambia; mengine nimepata, mengine sijapata.  Cha muhimu ni kulimbikiza ushahidi wakati mwandishi anaandika kuhusu kitu.  Hilo nimejifunza graduate school kwenye falsafa ya taaluma ya historia.  Na sio lazima mtu awe mfuasi wa Buddhism kuandika kitabu cha Buddhism; kwa mtazamo huo, ina maana Mutahaba asingeweza kuandika kitabu cha Ali Migeyo. Fani ya historia inatupa hatua tunazoweza kufuata kutafuta nyaraka, kuchambua, na kuandika.  Kwa ujumla ninachosema ni kwamba, baadhi ya vitu nilivyosoma, hoja itakuwa na nguvu zaidi pale kwenye vyanzo vingi (multiple source) vinavyosema kitu kimoja.  Kama chanzo kimoja kinasema hili na vingine vingi vinasema lile, hapo kunakuwa na utata.

Pamoja na watu wengi uliowataja wewe kwamba historia zao hazikuandikwa, kwanini historia za hawa wa miaka ya arobaini, hamsini pia hazijaandikwa.. Stephen Mhando, Kirilo Japhet, Dr. Joseph Mtangarwa, Dr. Kyaruzi, Dr. W.E.K. Mwanjisi, huyu Mzulu mwingine kutoka Afrika Kusini aliyekuja Tanganyika-Henry Muli, Godfrey Kayamba, na wengine?  Hawa nao historia zao zilizimwa?

Mohamed Said Salum ni sawa Schneider Plantan alikuwa ni mdogo wa Thomas Plantan na mwingine kwenye hii familia Mashando Plantan ndio alikuwa editor wa "Zuhra." Schneider alifungwa kwa propaganda za Wajerumani. Document niliyoona inasema Kleist Plantan (Abdallah Kleist Sykes) katoka South Africa na ndie alikuwa baba wa Abdulwahid, Ally, na Abbas. Hii inaweza kuwa imekosewa.  Kama nakumbuka wewe uliandika Sykes Mbuwane ndio katoka Afrika Kusini na yeye ndiye aliyekua baba wa Kleist Plantan

Prof. Mbughuni☝🏿

Azaria unaweza kupata historia ya Sykes katika Modern Tanzanians na John Iliffe Ed. East African Publishing House 1973, Daisy Sykes Buruku, Kleist Sykes The Townsman, pia The Life of Kleist Sykes, Seminar Paper, 1968 University of Dar es Salaam, History Department, East Africana. Sykes Mbuwane habari zake zote utazisoma humo. Aliyetoka Mozambique ni Sykes Mbuwane na Affande Plantan kwa jina lingine Mohosh. Hawa walikuwa chini ya Kamanda Herman von Wissman. Aliyekuwa mhariri na mmiliki wa Zuhra ni Ramadhani Mashado Plantan. Kuhusu Mwalimu Stephen Mhando yeye 1952 hakuwa katika uongozi wa TAA. Kipindi hicho viongozi walikuwa President Dr. Vedasto Kyaruzi na Secretary Abdulwahid Sykes. Katika uongozi wa Abdul toka 1950 hadi alipoingia Nyerere katika TAA 1953 kama President na Abdul Sykes akiwa Vice-President hali ilikuwa shwari. Nifahamishe ni Plantan yupi katika hawa ndugu watatu aliyefungwa kwa hilo kosa la kupokea mali ya wizi.

Sasa katika kipindi hiki cha uongozi wa Kyaruzi na Abdul, Abdul alitengeneza kitu kilichoitwa TAA Political Subcommittee na Stephen Mhando alimtia ndani ya kamati ile. Wajumbe wengine walikuwa Sheikh Hassan bin Amir aliyekuwa Mufti wa Tanganyika, Sheikh Said Chaurembo Hakimu Mahakama ya Kariakoo, Hamza Kibwana Mwapachu, Dr. Kyaruzi na John Rupia.

Kamati hii ndiyo iliyoandika mapendekezo ya katiba ya Tanganyika  aliyopelekewa Gavana Edward Twining 1950 na ilijadiliwa katika mkutano wa kuasisi TANU 1954. Baadhi ya mapendekezo ya hii document yalitiwa katika hotuba aliyosoma Nyerere UNO 1955.

Mohamed Said Salum Asante.  Kipindi hichi cha miaka ya hamsini bado nakipitia juu juu tuu, sijakipitia vizuri.  Nitaanza kukipitia vizuri na kukichambua nikimaliza project zingine.  

Nimerudi kwa haraka haraka kupitia hapo juu kwamba walimtoa Mhando mwaka 1952, lakini ni 1951 (Angalia attachment ya 1951). 

 Kulikuwa na makundi ndani ya TAA na udini ulikuwepo kabla ya 1953.  Na pia naona kuna vikundi/sects tofauti vya Waislamu vilikuwa vinakwaruzana miaka hiyo 1949-53.  Kulikuwa na Ahmadiyya, Ishmalia, Anjuman Islamia, Sunni, Shia, Arab Association, na vikundi/sects nyingine.  Abdulwahid Syke alijaribu kuongea na baadhi ya hizo sects. 

Swali langu kwako ni hili: kwenye nchi yenye watu wa imani tofauti na makabila tofauti, kama dini ingechanganywa na siasa wakati wa kugombea uhuru kukawa na vikundi vya Waislamu wa sect tofauti, vikundi tofauti vya madhehebu ya kikristo, vikundi vya kabila tofauti, matokeo yake leo yangekuwa nini kwa Tanzania?

Prof. Mbughuni☝🏿

Azaria nimeiona attach ahsante sana lakini hayo hayawezi kuwa yalipitika 1951 au 1952. Hayo yatakuwa 1950 kurudi nyuma kama nilivyokueleza. Hili mosi pili hivyo vikundi ulivyosema vikisuguana hili nakuhakikishia si kweli na nitakupa sababu. Ukitoa hao Kadiani ambao ni mchanganyiko wa Waafrika na Wahindi jumuia zilizobakia zote ni za Waasia na hawa hawakuwa na ugomvi wowote na mainstream Muslims. Hili pili. Tatu ni kuwa katika hili la kupambana na ukoloni hao wengine unaowataja walikuwa nje ya ulingo kabisa hawakuwa na nguvu yoyote. Nne na hili ndilo muhimu kuhusu Uislam katika mapambano haya wazee wetu walijua fitna ambayo  Waingereza wangeweza kuitia katika TANU kwa ajili hii Mufti wa Tanganyika Sheikh Hassan bin Amir na pia Khalifa wa Tarika  Qadiriyya alimuunga mkono Nyerere waziwazi. Tano, 1953 kabla ya Nyerere kuingizwa katika duru la inner circle pale New Street Abdul alikwenda Nansio kwa Hamza Mwapachu akifuatana Ali Mwinyi Tambwe Katibu wa Al Jamiatul Islamiyya kwenda kutaka ushauri juu ya Nyerere kuhusu kumchagua kuwa rais katika uchaguzi wa 1953 kisha 1954 waunde TANU. Kauli ya Mwapachu kwa Abdul ilikuwa ni muhimu Nyerere achaguliwe kuwa rais iundwe TANU na kudai uhuru. Akasema kumwambia Abdul ikiwa yeye Abdul atachaguliwa rais na TANU ikaundwa na kudai uhuru, hili jambo litachukuwa sura ya kuwa harakati za uhuru ni za Waislam. Nadhani umeelewa. Katika uchaguzi ule 17 April 1953 pale Arnautoglo Nyerere alimshinda Abdul kwa kura chache sana. Katika kitabu cha Abdul Sykes nimeeleza uchaguzi huu kwa kirefu sana. Siku zote inaandikwa kuwa Nyerere alichukua uongozi wa TAA 1953 lakini haielezwi uongozi huu aliuchukua kutoka kwa nani. Hofu ni ile ile ikielezwa kuwa alichukua kwa Abdul Sykes yatakuja maswali mengi.

Lakini juu ya tahadhari zote hizi Uislam ulitumika kama silaha ya kupambana na Waingereza na angalia historia ya uhuru ni nani waliokuwa na Nyerere.


Labda nami nikuulize swali. Iweje leo tuko hapa tunajadili historia hii kutokana na Abdul Sykes kufutwa katika historia ya TANU na uhuru wa Tanganyika?

Kama tukisema Abdul Sykes alifutwa kwenye historia, pia tukubali kwamba wengine kama wakina Dr. Kyaruzi, Mhando, Mwinjisi, na wengine nao walifutwa.

Prof. Mbughuni☝🏿

Asaria historia ya Abdul Sykes na Nyerere ni nyingine kabisa. Wala mimi si mtu wa ubishi. Mimi nimeandika yale niyajuayo kuhusu huyu baba yangu. Sijakulazimisha hata uniamini kama nasema kweli. Uko huru kuamini utakacho na upendacho. Hata hivyo kitabu cha Abdul Sykes sasa kina miaka 20 karibu toka kichapwe na tuko katika toleo la nne. Wewe si wa kwanza kuumizwa na kuchomwa na historia hii. Wako waliokusanya magazeti na kuyatoa katika mzunguko yasisomwe. Wako walotisha watu nk. Hakuna jipya katika historia hii ambalo mtu atakuja kunihoji ikawa hilo swali sijalisikia kabla.

No comments: