Hapo chini ni nyumba ya Bi. Fatima Matola mwanachama wa TANU
mazalendo aliyepigania uhuru wa Tanganyika.
Baba wa Taifa alikuwa akifikia nyumba hii wakati wa kupigania
uhuru.
Nani keshapata kusikia jina hili la Bi. Fatima
Matola?
Kuna hotuba ya Baba wa Taifa anasema kuwa safari
yake ya kwanza baada ya kuundwa TANU mwaka wa 1954 alikwenda Mbeya.
Lakini Nyaraka za Sykes zinaonyesha kuwa safari
ya kwanza ya Baba wa Taifa ilikuwa Mororgoro akifuatana na Zuberi Mtemvu.
Kuna barua ya tarehe 15 Agosti, 1954 mwezi mmoja
tu baada ya kuundwa TANU kutoka kwa Mtemvu akimwandikia Ally Sykes,
Mtemvu akieleza matatizo waliyoyapata yeye na Nyerere Morogoro katika
kuitangaza TANU.
Hii ndiyo safari ya kwanza
ya Baba wa Taifa katika kuitangaza TANU na safari ya pili ilikuwa Lindi.
Ikiwa safari hii ya Mbeya
kwa namna yoyote ilikuwa ndiyo ya kwanza basi Baba wa Taifa alifikia
nyumbani kwa Bi. Fatima Matola ambae nyumba yake ndiyo hiyo hapo chini kwenye
picha.
Kuna mtu yeyote anaemfahamu shujaa huyu wa ukombozi atupe historia yake?
Kuna mtu yeyote anaemfahamu shujaa huyu wa ukombozi atupe historia yake?
![]() |
Picha kwa hisani ya gazeti la Tanzania Daima Jumamosi Oktoba 14, 2017 |
No comments:
Post a Comment