Sunday 15 October 2017

MCHEKESHAJI WA BARZA YA MFALME (COURT JESTER) ANAPOMFEDHEHESHA MFALME MBELE YA WAGENI WAKE


Enzi za Ulaya ya Kale (Medieval Europe) kulikuwa na watu katika mabaraza ya wafalme kazi yao kubwa ilikuwa kumstarehesha mfalme kwa kumchekesha na katika kufanya hivyo kulichekesha barza zima. 

Wachekeshaji hawa walikuwa wanaitwa, ‘’Court Jesters.’’ 
Hawa walikuwa wachekeshaji tu na wakiendesha maisha yao kwa kazi hiyo ya kuchekesha. 

Kujipambanua walikuwa wana mavazi yao maalum ya kazi yao hiyo. 

Kama ilivyo kazi yao walioajiriwa walikuwa pia na mavazi yanayoendana na taaluma hiyo nayo ni mavazi ukiyaangalia tu mwenyewe unacheka. 

Nimeweka picha hapo chini kumwonyesha mchekeshaji wa mfalme alikuwa anaonekanaje. 
Court Jester alikuwa hana madhara katika jamii ukiacha ile kuwaumiza watu mbavu kwa kucheka.



Mchekeshaji katika Barza ya Mfalme
(Court Jester)



Lakini siku hizi pia wapo Wachekeshaji wa Mfalme, yaani, ''Court Jesters.''

Hawa kwa kuwa  dunia hii ya leo hakuna tena Barza za Wafalme utawakuta katika vyama vya siasa wakijikomba kwa wakubwa. 

Humo ndani ya vyama vya siasa ndimo walikojenga mabarza yao siyo ya uchekehaji bali ya fitna. 
Hawa hawachekesheshi watu bali hawa wanawafurahisha baadhi ya viongozi kwa namna ya kipekee.

''Court Jesters,'' hawa kazi yao kubwa ni kuwashambulia kwa maneno makali wale ambao wanaonekana wako dhidi ya ‘’Mfalme,’’ kwa kutumwa au wakati mwingine kwa kujituma wenyewe.

''Court Jesters,'' wa kale kazi yao ilikuwa ni kuchekesha hawa wa leo kazi yao ni kuumiza hisia za watu kwa maneno yanayochonganisha na kuvunja misingi ya umoja na utangamano. 

Kazi hii kwa hakika ukifanya uchunguzi wa kuwaangalia, ''Court Jesters,'' waliopita utagundua kuwa inahitaji mtu kuwa kidogo umepungukiwa katika uwezo wa fikra. 

Wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika kulikuwa na Rashid Sisso lakini huyu hakumdhuru mtu kazi yake ilikuwa kumchangamsha Nyerere katika mikutano ya hadhara na kwa kufanya hivyo kuiamsha hadhira pia isikize nini TANU inasema kama ujumbe kwa wananchi.

Hawa, Court Jesters wa leo hawako hivyo wameelemewa katika fitna na ili uiweze kazi hii sharti moja ni kuwa uwe hodari katika somo la farka.

Vinginevyo kazi hutaiweza. 
Itakushinda

Hii ni mfano wa yule mtu mfupi katika, ‘’circus’’ yaani, ‘’midget,’’ Kiswahili anaitwa, ''kibushuti.''
Ili uweze kuwa, ‘’midget,’’ katika, ‘’circus,’’ lazima uwe huna kimo, uwe kajitu kafupi na kadogo - kibushuti. 

La imetokea ulikuwa, ‘’midget,’’ kisha kwa rehma za Allah ukajaaliwa kuwa na urefu wa mtu wa kawaida mwenye, ‘’circus,’’ yake atakufuta kazi kwa kuwa huna tena ile sifa ya kuwa kichekesho.

Utakuwa umepoteza mvuto kwa watazamaji kwani wewe si kibushuti tena.
Angalia hiyo picha hapo juu. 

Huyu bwana kaalikwa katika hafla ya kutembelea meli kutoka Oman iliyokuja kupalilia udugu baina ya wananchi wa Oman na Zanzibar. 

Labda kuwa kuogoapa asije akawa kama ‘’midget,’’ aliyerudi kuwa mtu wa kawaida akaona ni muhimu kunigia katika meli hiyo akiwa katika mavazi yake anapokuwa kilingeni akistarehesha, na kumburudisha mfalme. 

Kaingia melini kavaa mavazi yake ya kazi.

Kawavalia waliomwalika kanzu yenye rangi ya chama chake.
Aliona ule ni uwanja stahiki wa kufikisha ujumbe wake. pale.

Wakubwa zake wanaipeleka saa mbele yeye kashika mishale anairudisha nyuma tena kwa kuipiga nyundo nzito.

Hakika huyu ni  Mchekeshaji wa Mfalme, ''Court Jester,'' katika ubora wake.

Midget
(Kibushuti)

No comments: