Wednesday 18 October 2017

KUTOKA JF: MAANDAMANO YA KWANZA ZANZIBAR 1989 BAADA YA MAPINDUZI


John...
Hotuba ile ya Sophia Kawawa ni moja katika misiba mikubwa iliyowafika
Waislam wa Tanzania.

Baada ya Sophia Kawawa kusema maneno yale katika ile hotuba yalifanyika
Maandamano makubwa Zanzibar ya kumpinga na mtu mmoja aliuawa na askari
walioamrishwa kuyazuia na wengine kadhaa katika waandamanaji kubakia vilema.

[​IMG]

Waandamanaji hawa walifikishwa mahamani na ilifanyika kesi iliyogusa
hisia za Waislam wengi Tanzania.

Mshtakiwa aliyetia fora kwa majibu yake mahakamani alikuwa Sheikh
Said Gwiji 
ambae alikuwa katika wakati ule ni mwanafunzi wa Sheikh
Nassoro Bachu 
kati ya masheikh vijana maarufu Zanzibar wakati ule.

Sheikh Gwiji na wenzake walihukumiwa kifungo sikumbuki miaka mingapi 
lakini ni zaidi ya mwaka na walitumikia kifungo kile.

Nilifanya mahojiano na Sheikh Gwiji nyumbani kwake Zanzibar mwaka wa
2012 kwa ajili ya kipindi cha TV Imaan Zanzibar na kisa hiki cha Sofia
Kawawa 
alikieleza kwa kirefu.

[​IMG]
Kushoto Sheikh Said Gwiji akifanya mahijiano na Mwandishi

No comments: