''Anaandika,'' Ridhwani Kikwete
Serikali yetu isipobadilika miaka yake (5) mitano itaisha kwa kufanya Uchaguzi kila mwezi.
Maana suala la chaguzi za marudio kila kuitwapo leo limegeuka kuwa Big Deal kwa CCM kwa minajili ya kufanya Spining.
Wakati wananchi hawana uhuru kupata habari za Bunge live kwa kisingizio cha kubana matumizi, leo gharama za kuendeshea, uchaguzi wa marudio Kinondoni peke yake unaigharimu serikali 1 bn Tsh.
Hata kama wabunge na madiwani wa upinzani wanakipenda sana chama chetu na wanatamani sana kumuunga mkono Mhe Rais John Pombe Magufuli, hebu tusiwapokee, tuwaambie "Kaeni huko mtahamia 2020" ili fedha hizi tuzipeleke kwenye miradi ya maji, umeme, na elimu.
Leo hii wananchi wangu wa Chalinze hawajui ni lini dawa zitaletwa kwenye Zahanati, Vituo vyao vya Afya na Hospital za Rufaa, lakini Kila kukicha ni habari ni chaguzi za marudio.
Hebu CCM tujitathmini sana na huu muda tunaoupoteza kila mwezi kufanya chaguzi za marudio, wananchi wana akili wanayaona haya. Tusipobadilika sasa 2020 watatuhukumu.
Ridhiwani Kikwete
22nd Jan - 2018
Kuna watu unapowasoma katika hii mitandao ya jamii zile elimu zao za juu na vipaji ambavyo si vya kawaida vinajitokeza dhahiri lakini katika kasoro.
Nimesoma maneno aliyoandikwa mwandishi hapo juu akimtilia Mh. Ridhwani maneno ya kuzua katika kinywa chake. Ujuzi wa lugha na somo lenyewe la sayansi ya siasa hauna wasiwasi katika yale yaliyoandikwa.
Lakini swali la kujiuliza ni kwa nini mtu anafanya hivi?
Kuna tija gani katika propaganda na uongo kama huu?
Ninachoweza kusema ni kuwa na yeye katuletea Watanzania, ''Ridhwani Effect,'' ya kwetu.
Huyu mtu aliyeweka yale maneno akidai kaandika Ridhwani ni bingwa wa propaganda. Bingwa kwa kuwa alijua Ridhwani atakanusha. Akajua pia kuwa vyote vyote itakavyokuwa msomaji akisoma kanusho atataka vile vile asome hicho kinachodaiwa kimeandikwa na Ridhwani. Sasa hapa ndipo yeye alipopataka yaani habari ienee na uzito wa habari hiyo ni ile mantiki iliyokuwa ndani ya ujumbe ule kuwa fedha zinapotezwa kwa mambo yasiyokuwa na umuhimu. Staili hii ya mambo kuenea inaitwa, "Streisand Effect." Google hiyo kupata mkasa mzima wa Barbra Streisand...

The Streisand effect is the phenomenon whereby an attempt to hide, remove, or censor a piece of information has the unintended consequence of publicizing the information more widely, usually facilitated by the Internet.
No comments:
Post a Comment