Mwinyi Baraka Sayyid Omar bin Abdalla |
Sayyid Omar bin Abdalla ni kati ya wasomi wachache aliosoma katika vyuo vikuu mbalimbali akapata shahada ya elimu zote mbili za dunia na akhera. Alianza masomo yake ya juu katika Chuo cha Makerere, kisha akenda kusoma Uiengereza Cho cha Oxford na kusoma katika baadhi ya nchi za Kiarabu kwa kuendelea kusoma. Alikuwa mhubiri mkubwa wa dini ya Kiislamu duniani kote aidha alipohama visiwani Zanzibar alipewa hadhi ya kuiwakilisha kisiwa cha Comoro katika masuala ya dini nchi za nje na mwishowe alikuwa ni mwakilishi wa Jumuia ya Kiislamu ya Saudi Arabia hadi anafariki. Nitaanza na maneno haya ya kimombo “In the popular mind love is usually linked with romance and sex. I never imagined that the first person I would fall madly in love with would be a short, flamboyant, erudite, bespectacled, snaggletoothed black man from Zanzibar who spilled things, wore long coats over a sarong, spoke in rich Edwardian English, had infection laugh and walked with a cane.”
Maneno hayo yamesemwa na Michael Sugich katika kitabu Sign on the HorizonsMeeting
with Men of Knowledge and Illumination. Tafsirii ya juu juu mapenzi ya
mtu kwa mtu mwengine huwa ya kijinsia lakini Michael Sugich ni kinyume anasema
hajakutana na mtu akafikia kuwa anampenda kuwa naye kama Sayyid Omar bin
Abdalla, msomi ambaye amebobea, mwenye kuvaa kanzu na majuba, mzee wa
Kiafrika kutoka visiwa vya Zanzibar ambaye huzungumza mombo lilokamilika la
mtindo wa Edwardian.
Sayyid Omar bin Abdaala (Mwinyi Baraka). Unapotaka kuwalinginisha Sayyid Omar bin Abdalla na Sheikh Abdalla Saleh
Farsy kuna sehemu wanakutana na kuna sehemu wanaachana. Wote wawili
walibobea katika elimu ya dini na historia, Sheikh Abdalla Saleh Farsy kaandika na
kutoa mawaidha, Sayyid Omar bin Abdalla hakuandika ila sehemu ndogo kabisa ya
makala kama kwenye Jarida la Mazungumzo ya Walimu Jarida ambalo walimu wa
visiwani Zanzibar wakiandika na kutoa maoni yao na maelezo mbalimbali. Sayyid
Omar Abdalla kenda kusoma katika vyuo Vikuu, Sheikh Abdalla Saleh Farsy
amesoma kwa Masheikhe mbalimbali, wote walipata kuwa walimu wakuu katika
chuo cha Kiislamu kiitwacho Muslim Academy, wote wawili wakitoa mawaidha ya
wiki katika radio ya Sauti ya Zanzibar. Sheikh Abdalla Saleh Farsy alikuwa Kadhi
alipokuwa Visiwani Zanzibar na Mombasa Kenya, Sayyid Omar bin Abdalla yeye
alikuwa Balozi na Dai mkubwa wa kuzunguka dunia nzima katika mabara yote
katika kulingania Uislamu amesafiri zaidi ya nchi 80 duniani kote.
Jina kamili la Sayyid Omar bin Abdalla ni Sayyid Omar Abdalla Abi Bakr bin
Salim, mzaliwa wa visiwani Zanzibar ingawa wengine huelezea kuwa amezaliwa
katika visiwa vya Comoro akiwa yatima alipelekwa visiwani Zanzibar katika mwaka
wa 1923 na kukulia na kusoma Unguja. Kumbukumbu katika faili lake binafsi
katika Ofisi za Nyaraka (ZNA AB 86/47) linathibitisha kuwa kazaliwa Zanzibar
katika mwaka wa 1918 na aliwahi kuthibitisha mwenyewe kuwa amezaliwa Zanzibar
katika mahojiano na Shirika la TV ya Kenya, KBC.
Ameanza masomo yake ya Qur‟an akiwa kijana mdogo alipojiunga na chuo
cha Maalim Abd al-Fatah Jamal al-Leyl maarufu Sharif Aboud. Mwalimu huyu
alikuwa akifundisha wanafunzi wake kuhifadhi Qu‟ran kwa kadri wawezavyo na
baadhi ya wanafunzi waliopita hapo waliweza kuhifadhi Mshafu mzima katika kipindi
cha baina ya miaka 3 na 5. Shariff Abbud alimuingiza Sayyid Omar Abdalla ambaye
kwa jina jengine akiitwa Mwinyi Baraka kujifunza Usufi na kujifunza juu ya Tarika ya
Qadiriyya.
Kama ilivyopata kuwa dasturi ya watoto wa visiwani baina ya sala ya Magharibi
na Isha huwenda kujifunza elimu mbalimbali juu ya Uislamu kwenye uga wa Fiqhi,
Tafsiri, lugha ya Kiarabu, Hadithi za Mtume Muhammad (SAW), Sira na fani
nyenginezo, Sayyid Omar bin Abdalla alikwenda katika Misikiti mbalimbali akiwa
kijana mwenye umri mdogo kwenda kusoma fani mbalimbali. Alikuwa akipenda
kujua mashairi ya Kiarabu na kujifunza kusomna Maulidi. Alionyesha uwezo
mkubwa wa kudhibiti alivyosomeshwa na haya yalikuja kuoenekana hata ukubwani
mwake uwezo wake wa kuhifadhi ulikuwa mkubwa sana na nafasi yake ya kusoma
ilikuwa ndogo mno na alikuwa akipenda kulala sana, ndipo wakati mmoja
alipoulizwa na Michael Sugich kwanini akipenda kulala sana akamjibu kwa mkato
“Unapolala huwa unaepukana na dhambi kwani huwa huna ulitendalo.”
Sayyid
Omar akipenda maneno ya mkato na kukufanya upende kumuuliza ili upate
maneno ya ufasaha na jawabu muwafaka.
Alipofika umri wa kijana alisogea kwa Sayyid Omar bin Sumayt wengine
wanaelezea alijifunza Tariqa ya Shadhiliya kwa Bin Sumayt.
Katika mwaka wa 1928 alisoma GCS ikiwa ni Government Central School
ambapo alimalizia darasa la 8 kisha akaendelea masomo ya sekondari GSS ikiwa ni
Government Secondary School, alikuwa kati ya wanafunzi wa mwanzo kuingia skuli
ya sekondari chini ya mwalimu Hollingsworth na kote alikosoma alikuwa ni
mwanafunzi anayofanya vizuri katika masomo yake, alisoma kwa miaka 3 masomo
ya sekondari ingawa kwengine kunaonyesha kuwa alisoma kwa miaka 4 hadi mwaka
wa wa 1936. Alielekea kusoma masomo ya Diploma katika Chuo Kikuu cha
Makerere kiliopo Uganda katika mwaka wa 1939, alianza kusomea uwalimu kwa
miaka 2 na mwaka wa mwisho ukiwa mwaka wa 3 alitakhasusi na somo la elimu ya
viumbe (Biology), Sheikhe huyu ndio aliokuwa mwanafunzi wa mwanzo wa visiwani
kupata shahada ya somo la ''Biology” na elimu hio ilikuja kumsaidia sana katika
kutoa mawaidha hasa akielezea elimu ya uzazi, suala la kutoamini Mwenye-enziMungu,
mabadiliko ya viumbe (evolution) na mwanzowake n.k.
Alipokuwa ansoma Chuo Kikuu cha Makerere huko Uganda, Sayyid Omar
Abdalla akicheza mchezo wa mpira na cricket na alikuwa na darsa akisomesha
wanafunzi wenzake wakati huo wakikuwepo kina Chief Abdalla Fundikira,
Marehemu Idrissa Abdul Wakil aliokuwa Rais wa awamu ya 4 wa Zanzibar, Spika
wa mwanzo wa Baraza la Wakilishi Zanzibar Ali Khamisi, Sheikh Ali Muhsin
Barwany, Maalim Zubeir Rijal, Mwalimu Abdulrasul Khako na wengineo, baadhi ya
wanafunzi wake katika darsa hizo wakimfanyia mzaha wakimwambia watamkimbia
kwani walipokuwa nyumbani walibanwa kutoweza kujifaragua na ujana wao na wapo
huko naye anawabana upande wake, Sayyid Omar akiwajibu „ujana ni sehemu ndogo
ya maisha, musipende kuendekeza.”
Sayyid Omar Abdalla katika Ujenzi wa Taifa, Ujenzi wa Uwanja wa Amani
Sayyid Omar Abdalla na walimu wenzake wa Muslim Academy. Aliporudi masomoni katika mwaka wa 1943 alianza kusomesha katika skuli ya
Dole wakati huo zikiitwa Rural Middle School (RMS) hapo alisomesha vijana wengi
ambao badaye walikuja kushika sehemu muhimu katika Serikali ya Zanzibar na
Tanzania kwa jumla, alimfundisha katika skuli ya Dole, Rais mstaafu wa wamu ya
pili ya Tanzania, Mheshimiwa Ali Hassan Mwinyi aidha akifundisha darsa katika
Msikiti wa Shariff Aboud.
Fatwana na mie na sehemu ya pili ya msomi huyu katika toleo lijalo...
No comments:
Post a Comment