Idd Suleyman Kikong'ona |
Amani iwe juu yenu.
Hakika wiki hii imekuwa ya majonzi na
maumivu makali ndani ya moyo wangu, ni wiki ambayo itakuwa ngumu kufutika
ndani ya kumbukumbu za maisha yangu. Nafsi imekumbwa na mitikisiko mikubwa
mitatu ndani ya wiki moja. Hii ni misiba iliyogonga moyo wangu. Maarifa yangu
ujuzi wangu wa kusarifu kurasa nami leo mmenifahamu kama Graphic Designer
mnayeniita mahiri na kunivika tuzo mbalimbali. Maarifa na Ujuzi ambao umejengwa
na kusimamishwa na nguzo kuu mbili.
Leo nguzo yangu kuu moja imedondonka.
Ni Idd Suleyman Kikong'ona ametangulia barzak. Sasa yupo mbele ya haki. Punde
tunamzika hapa Morogoro baada ya mshuko wa Swala ya Alasiri.
Huyu ni miongoni mwa magwiji wachache
wa fani ya Graphics mwenye upekee wa hali ya juu kuwahi kutokea ktk kitanga
hiki cha taifa hili la Tanzania. Hakika tumeondokewa na mtu muhimu kabisa.
Ingawa najihisi kama nipo kwenye
shimo lenye giza nene huku moyo wangu unalia, mwili wanitetema na nafsi haitaki
kuamini, lakini ndiyo mipango ya Mola mlezi.
Nimelikubali nimelipokea,
Nakuomba ewe Mola umlaze mahala pema
peponi, Ndugu yangu, kaka yangu, rafiki yangu, Mwalimu wangu IDD SULEYMAN
KIKONG'ONA.
Aamin.
Innaalillah'i Wainnaa Ilayh'i
Raajiu'n.
Ismael Abdoulkarym.
10/ Februari /2018
No comments:
Post a Comment