Ndugu Msomaji,
Fuatilia hapa In Sha Allah tutajitahidi kuweka mambo yanayosibu
nchi yetu toka tupate uhuru mwaka 1961...
Ninaandika kitabu kuhusu siasa za Tanzania na jinsi dini
inavyotawala hisia za watawala walio madarakani. Katika sura moja ninaeleza
namna Jakaya Mrisho Kikwete alivyoweza kufanya kampeni kwa miaka kumi na
hatimae akaweza kuchaguliwa kuwa rais...lakini haikuwa kazi nyepesi kwa mara ya
kwanza 1995 alipojaribu juhudi zake zilipata upinzani wa chinichini..
Nakuwekea hapa msomaji yale niliyoandika katika mswada wangu.
Nia ni kuangalia ni kweli Mwalimu Nyerere aliacha taifa lisilo na
udini, lenye mshikamano wa kweli na umoja?:
''But before the conference Kikwete went on
record to complain that the secretary of the party Dr. Lawrence Mtazama
Gama, a Catholic, and hailing from the south like Mkapa was
undermining his campaign on religious grounds.
Nyerere who had earlier
and eloquently promised him that he would take care of religious sentiments
for Kikwete, was suddenly dead silent.
For a time it seemed as if the party was to engulf into a
religious crisis involving its own top leadership. Religion was a sensitive
issue and CCM had always maintained that the party did not discriminate its
members on religious grounds.
The conflict between Kikwete and Gama was
an embarrassment to the party. In a strange turn of reconciliation effort
CCM issued a statement that Gama had apologised to Kikwete.
It is a pity that Kikwete did not reveal what
religious issue became the source of conflict that the party had Gama to
apologise.
The thought of Gama apologising to Kikwete was
a humiliation to Gama not only because of his seniority but
because of other factors...''
Hii ndiyo hali ilikuwapo wakati Kikwete na Mkapa wanaelekea
Dodoma kwenye mkutano wa Halmashauri Kuu ya CCM itakaochagua mgombea wa CCM.
Hapa Khalfan Mrisho Kikwete, Muislam alikuwa anakwenda
kupambana na Benjamin William Mkapa Mkatoliki mfuasi wa kanisa
lenye nguvu kupita kiasi Tanzania...
Fatilia ukarasa huu kwa mengine In Sha Allah...
''Mkapa was forced to pick his campaign committee from
people outside the inner circle of the party.
Two newspapers publishers were in his committee Damian
Ruhinda and Jenerali Ulimwengu.
The special NEC Conference convened to elect one CCM member to
stand for presidential candidate elected Jakaya Mrisho Kikwete in
the first round with Mkapa coming close second and Msuya was
last.
But since he had not commanded an absolute majority voting had to
be repeated.
There was tension in the conference hall as CCM delegates voted to
choose between Kikwete and Mkapa.
Christians were heard to whisper to each other that they should
not again allow a Muslim to govern the country, never again they whispered to
each other.
And when Mkapa won hymns were sung.''
Huu ndiyo ukweli wa siasa za Tanzania... dini haichezi mbali.
Lakini ili ndugu mfuatiliaji upate picha halisi ya nini kilikuwa
kinafanyika nyuma ya pazia itabidi nimlete mgombea mwingine aliyekuwa
mwanachama wa CCM...
Prof. Kighoma Abdallah Ali Malima...
''The difference between Prof. Malima and Kikwete was
that, while Kikwete really believed that he was a serious
candidate for Nyerere, Prof. Malima knew Kikwete was
thrown into the race by the Christian lobby to block him.
The rule of the game was to play a Muslim against a Muslim.
But Kikwete was too naive to understand that.
His background had not prepared him to understand the intricacies
of the politics of Tanzania as it relates to dealing with Islam and Muslims.
If he had taken some time to think long and hard he would have
realised that if experienced people like Malecela, Msuya and Kolimba were
not seen as fit to rule the country despite of their long service to the
country which span more than three decades how possible could he supersede them
and be a better candidate than those old guards?''
Marehemu Malima alikuwa akihadithia mkasa huu wa
mkutano wa Dodoma wa kuwafanyia usaili wagombea hakika akinitoa machozi kwa
kucheka.
Si kama yale aliyokuwa anahadithia yanachekesha hivyo bali kwa
vile mtu unavyoweza kushangaa inakuwaje watu wazima wakachezewa vile na Nyerere na
wao wasijijue kama wanachezewa.
Malima alikuwa
akinichekesha pale alipokuwa anasema yeye alipoingia kuhojiwa kamkuta Nyerere yuko
ubavuni kwa Mwinyi utadhani wamekaa kiti kimoja.
Ilikuwa lazima Kikwete aletwe kugombea vinginevyo
wagombea wote wangekuwa Wakristo ukimtoa marehemu Prof. Malima.
Hali ingelikuwa vile ingekuwa lazima Prof. Malima wamchague
ama sivyo Waislam wangelikuwa hawamo katika mbio za kwenda Ikulu.
Sasa Nyerere hakuweza kucheza na shilingi
chooni.
Prof. Malima na Mkapa washindane...hakuweza
kutabiri matokeo kwani Prof. Malima akipendeza sana kwa umma
wa Waislam...sababu za kupendeza huko ni kuwa Prof. Malima allijtolea
kuiasa serikali kuwa kuna ubaguzi wa kidini dhidi ya Waislam nchini petu.
Turudi mwanzo tulikoanzia...
Rais Kikwete anasema,
''Mzee Nyerere yule ametuachia Taifa moja, lililoungana, lenye
umoja, lenye amani na mshikamano...'' (Mwananchi Ijumaa, Aprili 18, 2014).
Hiyo hapo juu ni picha ya ya nchi yenye amani na mshikamano?
Jibu utakuwanalo wewe msomaji.
Waislam bila kificho wametembea nchi nzima kuwaeleza wananchi kuwa
Tanzania inaendeshwa na Mfumo Kristo na Waislam wanabaguliwa toka uhuru
upatikane. Kwa kauli hiyo hapo juu ya Rais Kikwete ni kuwa
kapuuza kilio cha Waislam.
Kwake yeye hakuna dhulma na Waislam ni waongo kwani wao na
Wakristo wote wana fursa sawa. Kanisa linatumia vyombo vya ulinzi kama jeshi lake
binafsi. Waislam wanapigwa ndani ya misikiti na kufunguliwa kesi za kubambika.
Kovu la Mwembechai la mwaka 1998 bado halijapona. Waislam
wamesingiziwa kuwa ni magaidi na askari wemeingia katika vijiji vyao kuwapiga
na kuwaua na misikiti yao kuchomwa moto.
Haya yametokea Kilindi na jambo la kusikitisha vyombo vyote vya
habari vimekataa kuandika habari hizi.
Binafsi nimezungumza na vyombo vya habari vya kimataifa na kuwapa
picha za video kuonyesha unyama waliofanyiwa Waislam.
Wamekiri kuwa hakika dhulma imetendeka lakini hakuna hata chombo
kimoja kilichokuwa na ujasiri wa kufanya kitu.
Majuma mawili yaliyopita Masasi Waislam wameingiliwa msikitini
baada ya sala ya Ijumaa na kupigwa kwa kusingiziwa ati wamemtukana Yesu.
Baada ya kipigo hicho wamfunguliwa kesi ya uchochezi. Swali la
kujiuliza ni hili kwa nini Waislam hawapelekwi mahakamani ila sisi ni kupigwa
kisha ndiyo tunafikishwa mbele ya vyombo vya sheria?
Ndugu msomaji hii ndiyo amani aliyotuachia chembelecho Rais
Kikwete, Mzee Nyerere? Hili ndilo taifa moja, lililoungana,
lenye umoja, lenye amani na mshikamano?
Rais Kikwete kipi kinamfanya ajifanye kuwa haujui ukweli?
No comments:
Post a Comment