IDDI SULEYMAN KIKONG'ONA (A.K.A BRO.
KIKO)
Assalaam alaykum warahmatullaah
wabarakaatuh,
Nami nitabaaruk tanzia ya Bro.
Kikong'ona.... Innaa lillaahi wa innaa
ilayhi raajiuun! Mioyo inahuzunika na macho yanatoa machozi, hatusemi ila lile
ambalo Mwenyezi Mungu analiridhia...
Bro. Iddi Kikong'ona ametangulia
mbele ya haki... Brother kwa kweli alikuwa na ataendelea kuwa mfano wa kuigwa
kwa anayetaka miongoni mwa vijana wa Kiislamu, nimemjua Brother Kiko pale
Ubungo Islamic, tukiwa wanafunzi wa Ualimu wa sekondari yeye akiwa mtaalamu wa
graphic designing na typesetting ya Vitabu vya Islamic Knowledge ambavyo leo
tunavitumia...
Brother alikuwa ni Mwanafikra, mpevu
na makini sana... kila tukikutana lazima akuache na jambo la kuishughulisha
akili yako juu ya Dini yako na nafasi yako km kijana...
Alhamdulillaah, nilimpenda sana na
alikuwa akinipenda sana, nakumbuka ndiye mtu wa mwanzo kunipa seti ya DVD za
"2 weeks Da'awah Program" za Sheikh Khalid Yasin na kwazo Vijana
wengi wa Ubungo Islamic wa wakati huo walikuwa wakiitana "Akhy..." na
"Daa'e..." ikiwa ni reflection ya mafunzo yatokanayo na DVD hizo.
Brother Kiko, alikuwa ni mchapakazi,
kabisa alimuigiza Sayyiq Qutb, Abul Alaa Maududi, Prof. Maalik kupitia
maandishi yao (ambapo muda mwingi utamkuta na kitabu mkononi) na Mwalimu na
Mzazi wetu Kida'awah Sheikh Mohamed Qasim.
Al akhy Iddi Kikong'ona alikuwa
akipenda mambo yaende bila kuleta nyudhuru... wakati akiendelea na typesetting
anaprint baadhi ya kurasa na kuja darasani kutugawia... "Masheikh... au
"wanazuoni" km alivyopenda kutuita... "hebu pitieni hizi kurasa
kuzihakiki" na vitabu vya shule ya msingi utakuta jina "Mujtaba"
kwa kweli ni jina la mwanae... sisi tukisaidiana nae kutunga maswali ya mazoezi
na kuyahakiki ubora wake...
Hata baada ya Kuondoka Ubungo Islamic
na kwenda Munadhwamat bado Iddi Kikong'ona alikuwa ni kiongozi wetu ktk
harakati za kushape bongo za vijana wa Kiislamu.
Kifo cha Bro. Kiko, kiwe chachu ya
kuongeza juhudi katika medani ya Da'awah hasa kwa sie vijana wa Kiislamu.
Twamuomba Allaah aikubali juhudi
yake, amlipe pepo ya Firdaws na ampe kauli thaabit. Twamuomba Allaah nasi
atujaalie mwisho mwema, Aamiyn.
Al Akhy Iddi Kikong'ona, pumzika kwa
Amani, umeifanyia kazi kauli ya sheikh Mohammed Qasim, kwamba hapa Duniani
hakuna kupumzika, tutapumzika Barzakh... Allaahu Kareem, pumzika Kaka... innaa
lillaahi wa innaa ilayhi raajiuun.
Mwl. Abu Sumayyah Salah
No comments:
Post a Comment