Utangulizi
Aziz
Ali alifariki mwaka wa 1950 miezi michache baada ya kutoka kuhiji Makka. Hata
kwa mbali katika maisha yake haikumpitikia kuwa mali aliyoacha nyuma itakuja
kutumika katika kupigania uhuru wa Tanganyika kwanza fedha zake zikitumika
wakati wa TAA kisha TANU kupitia mwanae wa kwanza Dossa Aziz.
Itoshe kusema tu gari alilomnunulia mwanae Nairobi mwaka wa 1947 kama kiliwazo baada ya kukataliwa katika masomo ya urubani kwa kuwa ni mtu mweusi, ndilo Dossa alilitoa kwa TANU mwaka wa 1954 kwa ajili ya kumsaidia Mwalimu Nyerere kufanya kazi zake kwa wepesi.
Al Haj Aziz Ali akiwa na wanae kulia Hamza Aziz, Dossa Aziz na Ramadhani Aziz |
Aziz Ali
(Picha zote kwa hisani ya Rose Aziz mjukuu wa
Aziz Ali)
|
Aziz
Ali amekuja Dar es Salaam kutoka Tanga mwanzo wa Vita Kuu ya Kwanza (1914-1918) akiwa askari
katika jeshi la Wajerumani na baada ya vita aliajiriwa na Goa mmoja.
Mwajiri
wake alipoondoka nchini alimwachia Aziz Ali gari mbili na hizi ndizo alizokuwa
akifanyia biashara hapo mwanzo na kufungua kampuni ya ujenzi akaajiri mafundi.
Aziz Ali akiwa kijana |
Kwa
hakika jina lake hasa ni Ali Kidonyo.
Hili ndilo jina lake alilojulikana akiwa mtoto na kisha kijana kwao Tanga.
Hili
Aziz alipewa na watu wa Dar es Salaam kwa hisani na wema wake.
Yeye
alikuwa akitoa fursa kwa watu kumpa pesa kidogo kidogo kama malipo ya nyumba
alizokuwa anawajengea na alikuwa mtu akishindwa kulipa akimpa muda hadi
atakapoweza.
Nyumbani
kwake mwezi Mtukufu wa Ramadhani alikuwa akitandika nje majamvi na kufuturisha
hadi watu 100 asiowajua wakija wanafuturu na kuondoka.
Ndipo
wakamwita "Aziz" yaani "Mpenzi." Ikawa wakimtaja jina
wanatanguliza "Aziz," yaani "Kipenzi chetu Ali."
Kidonyo
jina hili la kwao Tanga likafa kabisa.
Aziz
Ali alikuwa mcha Mungu sana.
Alikataa
kumwanzisha shule mwanae mkubwa Waziri maarufu kwa jina la Dossa hadi kwanza ahitimu
Qur'an.
Hii
ikapelekea Dossa kuanza shule darasa la kwanza akiwa na miaka 14 akawa darasa
moja na Abbas Sykes mdogo wa tatu kwa rafiki yake Abdulwahid Sykes.
No comments:
Post a Comment