Monday, 2 April 2018

KUTOKA FB: DOSSA AZIZ

Mwalimu Nyerere akimtunuku medali Dossa Aziz
Ikulu Dae es Salaam 1985

Antar Sangali Mwaka 1993 ikiwa naandikia gazeti la Majira nimewahi kufanya mahojiano na Waziri Dosa Aziz nyumbani kwake kijijini Mlandizi. Katika mazungumzo yetu ,Dosa alimtupia lawama Mwalimu Julius Nyerere na kusema "Hana shukran".Story hiyo ilinipa shida ya kuitwa mara kadhaa mbele ya jopo la wahariri wangu akiwemo marehemu Rajab Makugwe "Bob"na sammy Makilla wakitaka kujua kama mwanasiasa huyo ametoa matamshi hayo.Hofu iliokuwepo ni kwamba uhaba wa vitendea kazi ulinikwaza. Sikuwa na Tape recorder yenye sauti ya Dosa.Nikawahakikishia wakubwa wangu kuwa story hiyo ina actuality,ni reality na truth hivyo sitaiingiza kampuni kwenye mashitaka. Gazeti siku ya pili yake hadi majira ya saa 7 likawa halionekani mjini.Story hiyo ilimfanya mwalimu kumtembelea Dosa haraka haraka nyumbani kwake.Alipofika mwalimu siku hiyo nami niikuwepo nje,nyuso za Dossa na mwalimu zilipotazamana kila mmoja nilimuona akitoa kitambaa mfukoni na kujifuta usoni,kisha wakaingia ndani kwa mazungumzo ya faragha
Mohamed Said Antar Sangali...ahsante sana kaka...
Manage


Reply2h

Reply2h
Mohamed Said Antar iko siku nimesimama pembeni karibu na Cetral Police Police niko pembeni ya Sokoine Drive ghafla namuona Dossa Aziz anapita yumo ndani ya Pick Up rangi ya njano. 
Mimi nikashtuka sana kumuona Dossa anaendesha gari mjini Dar es Salaam. Nilikwenda n
...See More
Manage


Reply31mEdited
Mohamed Said Salum Anta sasa tuje kwenye hiyo picha ya Dossa na Nyerere. Picha hii ilipigwa Ikulu siku Dossa alipopewa medali na Baba wa Taifa.
Manage


Reply10m
Mohamed Said Salum Tarehe 27 Aprili, 1985 Julius Kambarage Nyerere, sasa akijulikana kama Baba wa Taifa, katika sherehe kubwa katika viwanja vya Ikulu, alitoa jumla ya medali 3979 kwa Watanzania waliochangia katika maendeleo ya taifa. 

Kati ya wale ambao walipewa medali hizo alikuwa Sheikh Abdallah Chaurembo. 

Wazalendo waliotajwa ndani ya kitabu hiki (''The Life and Times of Abdulwahid Sykes...'') ambao walipigania uhuru wa Tanganyika, hakuna hata mmoja wao aliyekuwa katika orodha ile ya heshima. 

Baada ya siku chache kupita, Nyerere kama mtu aliyegutuka alimualika Dossa Aziz Ikulu. Dossa Aziz, wakati wa kudai uhuru wa Tanganyika alikuwa mtu maarufu, mwenye nafasi, na kujiweza sana. 

Sasa Dossa baada ya miaka kupita hakuwa akifahamika tena na ule umaarufu na utajiri wake ulikuwa umetoweka. 

Alikuwa akiishi maisha ya kawaida kijijini Mlandizi, maili chache nje ya Dar es Salaam. 

Katika sherehe ya faragha Nyerere alimtunukia medali Dossa Aziz, rafiki yake wa zamani.
Manage


Reply8mEdited
Mohamed Said Salum Soma hapo chini nini Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ameandika kuhusu Dossa Aziz...



Reply5m
Mohamed Said Salumfile:///C:/Users/yemen/Downloads/dossa%20aziz%20dodoma2%20(4).pdfhttps://www.facebook.com/photo.php?fbid=2752478418111837&set=p.2752478418111837&type=3&theaterImage may contain: 1 person

No comments: