1.
Sheikh Ally naingia Maktaba In Shaa Allah niweke
ilikuwaje Bunge likapitisha Sheria ya Ugaidi. Hiki ndicho kitanzi chetu. Ikiwa
ni ndefu someni taratibu kidogo kidogo. Muhimu ni kuwa tujue imekuwaje kuwa
tuko katika hali hii.
2.
Sheikh Ally hapo chini ni paper nzima lakini
nitanyanyambua sehemu muhimi In Shaa Allah na kuziweka hapa kwa wepesi wa
kuweza kusomeka.
4.
Kwa ajili ya uchache wa Waislam katika Bunge
Sheria ya Ugaidi ilipitishwa kwa haraka bila ya mjadala wa maana khasa katika
vipengele ambavyo kwa hakika vilikuwa ni vibaya kabisa.
5.
Mathalan mtuhumiwa wa ugaidi anaweza akauliwa na
hapatakuwa na kosa na vipengele kama hivi viko vingi.
6.
Waliopitisha Sheria hii ya Ugaidi walipitisha
wakijua kuwa sheria hii itakuwa silaha kubwa kwao katika kuurudisha nyuma
Uislam.
7.
Masheikh wetu wamekuwa wahanga wa sheria hii
pamoja na Waislam wengine.
8.
Kwa ajili ya uchache wa Waislam katika Bunge
Sheria ya Ugaidi ilipitishwa kwa haraka bila ya mjadala wa maana khasa katika
vipengele ambavyo kwa hakika vilikuwa ni vibaya kabisa.
9.
Mathalan mtuhumiwa wa ugaidi anaweza akauliwa na
hapatakuwa na kosa na vipengele kama hivi viko vingi.
10. Waliopitisha
Sheria hii ya Ugaidi walipitisha wakijua kuwa sheria hii itakuwa silaha kubwa
kwao katika kuurudisha nyuma Uislam.
11.
Masheikh wetu wamekuwa wahanga wa sheria hii
pamoja na Waislam wengine.
12.
In order to understand the Tanzanian political
environment and to appreciate and comprehend the impact of ‘terrorism’ as
defined by the United States, first we need to point out that this phenomenon
was and still is a problem which involves the government of the United States
and to a limited extent its allies. The shock of 9/11 forced the United States
to not only to include its allies in its war against terrorism but also other
governments not forming part of the United States geo-political sphere like
Tanzania.
13.
Islamophobia has always existed in East Africa
and nowhere in the region has it gained ground and lodged itself in the
political system as in Tanzania. The rise of Islamophobia in Tanzania therefore
did not need the bombing of the United States Embassy or 9/11 to bring it to
the surface.
14.
Tanzania passed the Prevention of Terrorism Act
of 2002, which in all intent and purpose replicated the United States Patriot
Act of 2001. Due to under representation of Muslims in parliament the Act
sailed through without any difficulties notwithstanding Muslim opposition
outside the parliament.
15.
On 17th May 2003 with the anti-terror
legislation in place the police in collaboration with the FBI (who were already
in the country waiting for the president to assent the bill) arrested Muslims
suspected to be ‘terrorists.’ But those arrested had nothing to do with
terrorism; they were Muslims leaders who the government arrested for being
‘opponents’ of the government and ruling party the Chama Cha Mapinduzi
(CCM). Among those arrested were leaders
of various Muslim charitable organisations - foreign oriented and local, who
have distinguished themselves in providing social services to Muslims like building
mosques, schools, orphanages etc.
16.
In response to these arrests Muslims staged a
mass demonstration against the government and the United States opposing the
mass arrests of the Muslim leadership, harassment by the local police, the FBI
and against the Anti – Terrorist Legislation.
17.
Baadhi ya mambo niliyonyanyambua kutoka hiyo
paper niliyotoa Chuo Kikuu Cha Ibadan 2006.
18.
The law empowers the Minister to freeze bank
accounts of any suspected ‘terrorist organisation’ or individual. Nowhere is
the law frightening than in part V 28 (6). This section deserves special
mention. It stipulates that:
19.
A police officer who uses such force as may be
necessary for any purpose, in accordance with this Act, shall not be liable, in
any criminal or civil proceedings, for having, by the use of force, caused
injury or death to any person or damage to or loss of any property.
20.Sheikh Mohammed Said, salaam!!
niwie radhi kwa kuchelewa kuiona hii, ila shukran kwa Allah nami nimeipata, ninaisoma
word to word and then In Shaa Allah, nitakuja tena kwaajili ya kuibua mjadala
au hata kuuliza maswali.
21.
Sheikh Ally karibu sana. Hiyo paper iliniponza.
Sponsors wa hiyo conference walikuwa Iran na US. US walikuwa na desk lao mbele
na opening yangu nilitaja nchi ambazo US wameua watu duniani - Laos, Cambodia,
Vietnam, Palestine silaha zao zinatumika kuua...jamaa wako pale na
representative wa United Republic of Tanzania alikuja kutoka Lagos na cameras
were rolling...US wakaleta taarifa Dar es Salaam kuhusu "terrorist
sympathiser." Mwaka unaofuatia 2007 narudi kutoka Tehran nilipoalikwa
mkutano nikakamatwa uwanja wa ndege kwa tuhuma za kusafirisha madawa ya
kulevya. Detained overnight na heavy interrogation baada ya upekuzi wa mizigo
yangu. Siku moja baada ya miaka 8 nikakutana na arresting officer wangu na yeye
ndiye alikuwa main interrogator. Akanivuta pembeni tukasalimiana. Ni kijana wa
Kiislam. Alichoniambia ni kuwa. "Brother you really impressed me in the
way you responded to our questions." Passport yangu imetiwa alama huwezi
kuiona kwa macho ila inatokeza katika computer za Immigration duniani kote kuwa
natakiwa kufanyiwa, ‘’extra security check before boarding.’’ Pili fedha zozote
ninazopokea kutoka nje huwa ‘’delayed,’’ siku mbili au tatu ndiyo napewa. Juu
ya haya yote nilialikwa US University of Iowa na Northwestern University
Evanston, Chicago Department of African History for public talk. Waamerika walinambia
hawakuwa wanajua ‘’role,’’ ya Waislam katika kupambana na Wajerumani, ‘’in
armed,’’ combat wala jinsi tulivyomweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere
katika uongozi wa nchi. Wakasema sasa wanaelewa kwa nini Waislam wanasuguana na
serikali. Alhamdulilah. Baada ya hapo wakanitia katika mradi wa kuandika
Dictionary of African Biography (DAB) uliokuwa chini ya Harvard na Oxford
University Press, New York. Mradi umekamilika na ni volumes 6. Alhamdulilah...
22. Waamerika
wana msemo, "There is no free lunch in Amerika." Wametaka kujua mengi
yetu nami nimewapa Elimu bila Khiyana.
1. Hawa watu huli dola zao bure ukialikwa unafanya
kazi kweli kweli na wanaheshimu utaalamu.
1. Pale Northwestern University nilizungumza kwenye
Ukumbi wa Eduardo Mondlane yeye alisoma pale na ndipo alipokutana na mkewe
msichana wa Kimarekani. Ukumbi umepambwa kwa vinyago vya Kimakonde. Sasa hawa
jamaa walikuwa wamenipangia Hilton kwa majuma mawili. Kabla sijaanza kuzungumza
nikawa nawatania nikasema, "You Americans are very kind and generous
people, why put me in such a posh place..." Akatokea mtu kwenye audience
anazungumza Kiswahili kama mtu wa Kariakoo, "Sikiza Bwana Mohamed wewe ni
mtu mkubwa bwana sasa unadhani sisi tukuweke wapi wewe!" Duu nilipigwa na
butwaa.
2.
New York. Nimekwenda ATM Chase Manhattan Bank
kutafuta senti. Nimetumbukiza Master Card yangu. Screen ikazimika ikawa blank
hakuna kinachoonekana. Nikasema sasa ndiyo naadhirika ugenini. Nikampigia simu
rafiki yangu Washington akanambia nitulie nisiwe na hofu ikiwa itagoma yeye
atanitumia fedha. Siku ya pili nikenda bank lakini kwanza nikenda counter
kueleza mkasa wa jana. Akaniambia nijaribu tena. Safari hii kutia card inasoma
na nikakamilisha muamala wangu. Nini kilitokea. Kumbe hata card zangu za bank
kwa ajili ya, "terrorist sympathiser," zilikuwa monitored na walitaka
kujua niko wapi na nachukua fedha kiasi gani...
3.
Duh!! Alhamdulillah kwa kushea nasi hii historia
yenye kuvutia...I am now asured that I will not be mistaken to calling you a
teacher of history, your very impresive histories inspire me.
4.
Doh!! habari habari nzito.
5.
Poyo Abeid: Sheikh Said, hivi umefikiria
kuandika auto biography?
6.
Poyo Abeid: Tunataka nawe sasa tukusome ukiwa
kinda mitaa ya Kariakoo, bandari hadi ugwiji wa historia hi ya kipekee
uifundishayo.
7.
Sheikh umeikaanga sana America, lazima upate
changamoto kila unapotaka kuingia kwao.
8.
Sheikh Abeid umenikumbusha kitu. Siku moja
yapata miaka 20 iliyopita niko na mwanangu wa kwanza tunatoka msikitini Maghrib
akanambia, "Baba mimi In Shaa Allah nikiwa mkubwa nataka niandike maisha
yako." Nikamwambia, "Mimi si mtu muhimu hakuna atakaetaka kusoma
habari za baba yako." Akanijibu kwa kusema, "Mbona watu wengi maarufu
wanakufata nyumbani?" Juzi asubuhi
kanipigia simu dada yangu mmoja simu baba yake alikuwa, ‘’financier,’’ wa TANU
akaniuliza kama ninafikiria kuandika histori ya maisha yangu...Ukweli ni kuwa
mie sina umuhimu wa kiasi hicho wakuandikwa ndiyo hawa siku zote tunawataja.
9.
Sheikh Ally kama kuandika fikra zangu za awali
sana si Kariakoo bali niko Moshi nina umri wa miaka 6 nina rafiki yangu
Gregory Georgoudis mtoto wa Dr. Gergoudis na mama yangu ni nurse
katika hopitali yake Moshi Nursing Home. Wagiriki hawa na Gregory na mimi umri
wetu ulikuwa sawa. Gregory anasema Kiingereza sasa jiulize tulikuwa tunaelewana
vipi? Rafiki yangu akiingia ndani akitoka na cake basi mbili moja yake moja
yangu...Huyu alinitoa uoga wa kutowaogopa Wazungu...sijui kwanini kichwa changu
kilikuwa kinakamata sana muziki...nikaa nje katika garden yao nikiwa peke yangu
muziki uliokuwa ukipigwa mle ndani kwao ulikuwa ukinichukua sana...Hii ilikuwa
1957/58.
10. 1957/58!!!!
mbali sana na umeweza kukumbuka matukio ya miaka hiyo??
11.
Sana...nina mjomba wangu Bwana Hamisi Salum yeye
ndiye mtu wa kwanza kuniingiza hoteli kula chakula na kunipakia kwenye baiskeli
na pia kuniingiza mpirani nikiwa na kama miaka 5 huwa namuhadithia yote na
anashangaa sana. Akinipenda sana na yu hai. Alikuwa na ubao wa biashara
Kariakoo Sokoni. Namhadithia alivyokuwa akinichukua pale sokoni akiniweka
pembeni yake na kutwa nzima ni kuninunulia vitu nakula-kumbikumbi wakipita
ananiagizia, njugu nk. nk. huwa namhadithia anachoka hadi mambo ya Ilala
Stadium na kunipakia katika njinga.
Huyu kijana anasema Kiswahili utadhani yuko Manzese na kajifunza Amerika. Mtume SAW kaeleza umuhimu ya kujifunza lugha ya kigeni, nimekuta vijana wanazungumza Khosa, Kizulu, Hausa... |
1.
Prof. Michael Lofchie (hapo juu) kaja Tanzania 1964 au 1965
kutafiti Mapinduzi ya Zanzibar akiwa na miaka 25. Katika rafiki zake alipokuwa
Dar es Salaam ya 1960s ni Ally Sykes. US Embassy iliomba serikali ya Tanzania
kuwa huyu kijana wao asibughudhiwe...ndugu zangu kuna mengi sana lazima
tuyajue...
2.
Kuna mmoja prof. ni mwanamke kaniuliza Mariam
Abdul Sykes hajambo? Nikamwambia amefariki. Akanambia nimesomanae darasa moja
Bunge Primary School yeye baba yake akisomesha University of Dar es Salaam.
Mbona nilikuwa hoi? Hawa ndiyo ndugu zetu walioko huko.
No comments:
Post a Comment