Kushoto: Salim Rashid, Abdulrahman Babu, F. Thompeon, Ali Mwinyigogo, David Kimche?, Abeid Karume, Abdallah Kassim Hanga, Aboud Jumbe, Idris Abdulwakil, Abdulaziz Twala |
Kushoto Netanyahu na David Kimche |
Nimeikuta
picha hiyo hapo juu katika group moja na chini yake huyo aliyeiweka akaandika
maneno haya: ‘’ Duh! Watu muhimu sana hawa katika historia ya Zanzibar!’’
Picha
hii naifamu na mtaalamu wa historia ya Zanzibar amepata kunieleza kuhusu huyo anaesemwa
kuwa ni David Kimche kuwa si yeye.
Mtaalamu
huyu akaongeza akanambia, ‘’Kimche hakai kupigwa picha, yeye anafanya mambo
wanakuja watu kupiga picha.’’
Kwa
wale wasiomjua Kimche, huyu alikuwa kachero mkubwa katika MOSAD Shirika la Ujasusi
la Israel.
Lakini
si kama Kimche hakufika Tanganyika na Zanzibar la hasha kafika kote wakati inafanywa
mipango ya kupindia serikali ya Sheikh Mohamed Shamte.
Kimche
alikuwa na watu wake Tanganyika wakijuana vizuri tu.
Kimche
wataalamu walimpa jina, "Master of Disguises." Kwani alikuwa na uwexo
wa kujibadili sura na umbo atajavyo.
Kimche
alipofariki miaka michache iliyopita magazeti mashuhuri ulimwenguni yalitangaza
kifo chake na kuandika taazia yake.
Turejjee katika maneno aliyoandika mweka picha, ‘’Duh! Watu muhimu sana hawa katika historia ya Zanzibar!’’
Katika picha ile ya watu kumi, wanane ni wananchi na katika hawa wanane watatu waliuliwa - Abdallah Kassim Hanga, Abdulaziz Twala na Abeid Karume.
Inawezekana umuhimu aliouona mweka picha ni hii hstoria ya kusikitisha ya mauaji.
No comments:
Post a Comment