UBAGUZI WA RANGI
ULIVYOMKUMBA DR. AGGREY UKIWEMO WA NEW AFRICA HOTEL ENZI ZA UKOLONI
Na Kamili Mussa
Dr. James Emmanuel Kwegyir Aggrey ni jina ambalo takriban 98%
ya Watanzania hawalijui wala hawajawahi kulisikia.
Dr. Aggrey, mghana aliyetokea Achimota Ghana, ingawa kwa sasa
ni marehemu, ni mwafrika ambaye bado anayeheshimika sana ulimwenguni licha ya
kufariki miaka karibu 100 iliyopita.
Dr. Aggrey ameacha historia kubwa barani Afrika ikiwemo
Tanzania. Katika maisha yake alikumbana na kila aina ya ubaguzi toka kwa wazungu.
Hapa Tanzania pia, ubaguzi wa rangi haukumuacha salama kwani
alikumbana nao katika hoteli maarufu ya New Africa Hotel.
Hoteli hiyo ya New Africa Hotel iliyopo maeneo ya posta
jijini Dar es Salaam, ilijengwa na Wajerumani baada ya kukabidhiwa Tanganyika
kufuatia Berlin Conference 1884-85.
Enzi za ukoloni wa Mjerumani na Mwingereza, ilikuwa ni
marufuku kwa Mwafrika kukanyaga hotelini hapo labda tu kwa kibali maalum au
kama ni mfanyakazi wa hoteli hiyo.
Dr. Aggrey alikuja Tanganyika mwaka 1924 kama Mjumbe wa
Phelps-Stokes Fund Commission kuja kuangalia jinsi ya kuwaendeleza Waafrika
kielimu. Dr. Aggrey alikuwa Mwafrika pekee kwenye Commission hiyo. Commission
iliundwa kutokana na Ms. Carolyne Phelps Stokes, ambaye alifariki mwaka 1909 na
kuacha kitita cha fedha, ($ 1,000,000) na usia uliosema- "I bequeath the
same to My trustees to be used for the education of Negros, both in Africa and
the United States, North American Indian and needy and deserving white
students".
Ni kutokana na wosia huu ndipo ilipoundwa Commission hiyo
ambayo ilizuru mataifa kumi ya Afrika. Commission hiyo ilizuru Tanganyika na
Zanzibar toka Machi 1924 hadi April 1924.
Baada ya Commission hiyo kuwasili jijini Dar es Salaam,
wajumbe waliamua kufikia New Africa Hotel, moja ya hotel chache kubwa na ya
kuheshimika nchini wakati huo.
Katika hali ya kusikitisha, Dr. Aggrey, akiwa Mwafrika pekee
katika Commission hiyo, alikataliwa kupewa chumba katika hotel hiyo ya kutokana
na Uafrika wake!
Hili jambo lilimuhuzunisha sana lakini hakukata tamaa na
akaendelea na harakati zake za kuwasaidia waafrika wenzake kwa kadri
alivyoweza. Baada ya kukataliwa chumba, ilimbidi
Dr. Aggrey akajitaftie chumba kwenye hoteli nyingine.
Dr. Aggrey, akiwa Dar es Salaam, ndiye aliyemshauri Kleist
Sykes kuunda chama kwa maana ndiyo inhekuwa rahisi kupigania haki zao kwa
pamoja. Kleist alikuwa kijana msomi mwenye kuzungumza Kijerumani na Kiingereza
fasaha. Ilimchukua Kleist miaka mitano kuunda chama kiitwacho African
Association (AA) hapo mwaka 1929 kwa minajiri ya kuwapigania Waafrika. African
Association baadae ilibadilishwa na kuwa Tanganyika African Association (TAA)
mwaka 1948. AA ndiyo iliyokuwa chimbuko la TANU iliyoanzishwa tarehe 7.7.1954.
Kutokana na wazo hilo muhimu kwa historia ya nchini yetu,
wahenga watakumbuka kuwa iliamuliwa Dr. Aggrey apewe mtaa jijini Dar es Salaam
kama kumbukumbu. Ndipo mtaa huo uliopo maeneo ya Kitumbini kuelekea Kariakoo,
jijini Dar es Salaam ukapewa jina la Mtaa wa Aggrey.
Dr. Aggrey alikuwa ni mwalimu mwenye utaalamu wa hali ya juu
aliyetambuliwa na kuheshimika duniani kote.
Mwaka 1895 akiwa Mwalimu wa shule ya Wesleyan Memorial
School, alifanya mtihani, pamoja na waalimu wengine 119 nchi nzima ya Ghana,
uliotungwa Uingereza. DR. AGGREY aliibuka Mwanafunzi Bora na ndiye pekee
aliyepata Second Class na kutunukiwa cheti maalum.
Cheti hicho alichotunukiwa na Malkia wa Uingereza
kiliandikwa-: "This Certificate of Distinction qualifies you, without
further examination, to teach in any similar school in any British colony, the
world over". Dr. Aggrey alikuwa Mwafrika wa kwanza kutunukiwa tuzo hiyo.
Commission hiyo, baada ya kutoka Tanganyika ilikwenda Belgian
Congo. Huko, baada ya shughuli ya siku nzima za siku ya kwanza, Gavana (mzungu)
akaialika Commission kwaajili ya Dinner, Ikulu. Gavana alipomuona Dr. Aggrey
akiwa na wajumbe wengine ambao walikuwa ni wazungu aliamuru asiingie ndani
hivyo akabaki mlangoni akiliwa mbu na kupigwa baridi hadi wenzake walipomaliza
dinner!
Figisu hizi hazilumkatisha tamaa Dr. Aggrey na badala yake
zilimpa nguvu zaidi kwani alielewa kuwa jukumu lake ni kuwasaidia Waafrika
kielimu. Baada ya hapo Commission ilikwenda Angola ambako masaibu ya ubaguzi wa
rangi yaliendelea dhidi yake ambapo kuna siku alichelewa kutoa mhadhara baada
ya kusukumizwa nje ya treni kwavile tu ni mweusi!
Commission hiyo baada ya hapo ikaenda Afrika ya Kusini ambako
Dr. Aggrey alitoa moja kati ya hotuba bora kabisa kuwahi kutolewa na Mwafrika
ambapo, kwa ufupi, alisema:
"By Education, I don't simply mean learning. I mean the
training of the mind, in morals and in a hand that helps to make one socially
efficient. Not simply the three R's, but the three H's ie the Head, the Hand
and the Heart. No race or people can rise half slave, half free. The surest way
to keep a people down is to educate the men and neglect the women. If you
educate a man you simply educate an individual but if you educate a woman you
educate a family."
"I am proud of my colour and whoever is not proud of his
colour is not fit to live. Keep your temper and smile. That is what Jesus meant
when he told men to turn the other cheek."
"I have no time for revenge that is not African. Some
white people ought to be transformed to Negros just for a few days, so as to
feel what we feel and suffer what we suffer. I prefer to be a Spokesman of my
entire country: Africa, My Africa".
"My fellow Africans, I dont care what you know; show me
what you can do. Many of you who get educated dont work, but take to drink. You
see white people drink so you think you can drink too. You imitate the weakness
of the white people, but not their greatness. You won't imitate a whiteman
working hard".
"If you play only the white notes on a piano, you get
only sharps; if only the black keys, you get flats. But if you play the two
together you get harmony and beautiful music".
Baada ya kutoa muhadhara huo White settlers walichanganyikiwa
kwa uwezo mkubwa wa Dr. Aggrey na na kiongozi wao akatamka-: Damn his colour,
he is a saint!
Dr. Aggrey alikuwa ni mjuzi wa mambo mengi lakini hobby yake
kubwa ilikuwa ni kusoma vitabu vya kila aina na alipenda kusema-: I want to
know everything". Alikuwa akijisomea hadi usiku wa manani. Aliposinzia,
alikuwaakichukua taulo akalichovya kwenye maji na kujifunga kichwani na kuweka
miguu yake kwenye karai la maji ya baridi ili aendelee kusoma vitabu vyake! Kwa
hakika, alipenda sana kusoma vitabu.
Dr. Aggrey alikuwa akiongea Queen's English na alipozuru US
kwa mara ya kwanza, wamarekani hawakuamini kama Mwafrika angekuweza kuongea kwa
lafudhi ile na kupelekea Waziri HEC Byrant aseme:
"He is dark as dark, but very few in America can use
English as he can".
Dr. Aggrey alifariki dunia nchini US tarehe 30 Julai 1927
kutokana na ugonjwa wa Meningatis na kuzikwa North Carolina, US.
Kwa heshima ya Dr. Agrey, mwaka 2017 nchini Ghana, picha
yake iliwekwa kwenye fedha ya nchi hiyo (5 Cedi Bill).
Huyo ndie Dr. James Emmanuel Kwegyir Aggrey mwenye mchango
mkubwa katika historia ya taifa letu.
No comments:
Post a Comment