Showing posts sorted by date for query chipukizi. Sort by relevance Show all posts
Showing posts sorted by date for query chipukizi. Sort by relevance Show all posts

Thursday, 22 February 2018


Kushoto Mwandishi wa Riwaya Mohamed H. Magora na Mohamed Said

Mohamed Magora ni mwanangu nimemuona akiwa mtoto akitambaa wakati nikienda kwao kwa baba yake kwa kazi za uandishi. Nikikaa katika varanda ya kwao na baba yake, Mohamed  mtoto mchanga akitambaa kwenye busati siku hizo kitoto kidogo kabisa. Sikutegemea kuwa iko siku Mohamed na mimi tutakutana uso kwa uso tena katika taaluma niipendayo ambayo na yeye pia kaipenda nayo ni uandishi. Lakini Mohamed kanishinda kwa kuwa mwenzangu, somo yangu yeye ni mtunzi wa riwaya zenye kusisimua sana tena zilizojaa mapenzi kitu kilicho aziz katika umri wa ujana kama huo wake.

''Baba nataka ukisome kitabu changu, baba kasema nikuletee.'' Mohamed huyo ananiambia baada ya kufika kwangu na baada ya mamkuzi.

Nimepigwa na butwaa kwani hata miaka miwili haijapita bwana mdogo huyu alikuwa kanipa kitabu chake cha kwanza, ''Masha Johari ya Kale,'' mara karejea tena kwangu na kitabu kingine. Ikanipitikia kuwa Mohamed si mwandishi wa kawaida na sioni kingine mbele yake ila In Shaa Allah mafanikio makubwa kwake katika uandishi.

Mohamed ni kijana hodari na fikra zake kazielekeza vizuri katika jamii anayoishi. Kalamu yake imelenga kwanza kwa vijana wenzake kueleza hali zao halisi katika ulimwengu huu wa usasa na kisha akageuza shingo upande wa pili kuwangalia wazazi wa vijana hawa jinsi wanavyohangaika katika kuwaelewa na kuwaelekeza watoto wao na pia kuelewa mazingira yanayowakabili. Kwa hakika ukimsoma Mohamed unapata picha ya mgongano wa nyakati, tabia, mwelekeo na mategemeo ya pande zote mbili ya watoto hawa wa kizazi kipya na wazee wao waliogubikwa na historia ya kale huku wakivutwa na mambo ya dunia hii ya leo. Mohamed anawasihi wazee wajaribu kuangalia mwelekeo wa dunia ya leo na changamoto zake.

Mwandishi Mohamed mwenyewe ana Kiswahili kizuri cha kuvutia unapomsikia akizungumza na halikadhalika ujuzi huu unaakisiwa katika kalamu yake. Mohamed katika kitabu hicho hapo juu anasema katika moja ya kurasa, ''...ajabu ya mbalamwezi kuanikia muhogo...'' Usemi  huu umenigusa pasipo kiasi kwani juu ya uzee wangu na umri wangu katika uandishi sijapatapo kusikia maneno haya na mimi  si mtu wa kucheza ngoma na mzigo kichwani katika dunia hii ya uandishi. Mzigo nimeutua uko chini. Naandika nikiwa sina hofu ya kuubwaga mzigo wangu.

Nashawishika kuuweka hapa utangulizi wa kitabu hiki, ''Chuo Kikuu ''Shaurimoyo,'' ili sote tufaidi kama mwenyewe mwandishi alivyoandika:

''Chuo Kikuu Shaurimoyo,’’ ni kitabu kinachosawiri uhalisia wa maisha ya wanafunzi wa Chuo Kikuu.

Ngazi ya elimu ya chuo kikuu huhesabiwa kuwa na dhima ya kufanya maandao ya maisha ya wanafunzi. Wanachuo hujifunza taaluma mahsusi walizochagua kwa hiari zao ili wazitumikie katika kuendesha maisha yao. Hujifunza maisha ya uhuru na kujitegemea, hujifunza namna ya kutangamana na wanajamii, hukuza ndoto zao za maisha na hivyo kuwa na kiu ya kujistawisha. Mambo yote hayo ni muhimu sana katika kujenga msingi wa kuta za ustawi kama yataendewa kwa nidhamu, uvumilivu, juhudi na maarifa.

Njia ya kuelekea katika kilele cha fanaka haipo tambarare wanachuo hukumbana na changamoto mbalimbali za kijamii zinazosogeza karibu hatari ya kudamirika kwa mustakabali wao. Changamoto za kimaadili hupelekea wanachuo kuathiriana na kujikuta wapo katika shimo la maangamivu kwa kuzama katika matendo yanayopambanulika kuwa ni haramu kama ulevi, kamari, na mambo mengine yanayokwamisha mafanikio.

Kitabu hiki ni cha kusomwa na wakubwa na wadogo kwani wote kwa namna moja au nyingine wameguswa sana humo ndani na naamini katika wasomaji wako ambao watakuja kusema, ‘’Ala, kumbe mambo ndivyo yalivyo?’




Thursday, 2 February 2017



Baada ya kusoma taazia ya Abdallah Tambaza sina nguvu ya kuandika chochote kuhusu rafiki yangu Mohamed Awadh maarufu kwa jina la Chico. Taazia ya Abdallah mimi imenitia simanzi kiasi ya machozi kunilengalenga kila ninapopita sentensi moja kwenda nyingine sababu ni kuwa Abdallah alikuwa ananitajia mambo na watu niliokuwa nawafahamu na wengine tayari wameshatangulia mbele ya haki. Nikawa kama vile watu hawa nawaona tena. Miezi kama miwili hivi nilikutana na Chico Masaki akiwa amekaa na wajukuu zake ndani ya gari. Tulisalimiana kwa bashasha sana na wala haukunipikitikia kuwa ile ndiyo itakuwa mara yetu ya mwisho kuonana. Mazikoni Kisutu nimekutana na Abdallah kisha nikamuona na ndugu yake Mwinyikhamisi yeye ni mkubwa kwangu kwa umri na aliponiona tu Mwinyikhamisi anahangaika kusimama maana alikuwa kakaa chini miguu inampa tabu. Kila nikimzuia kunisimamia yeye ndiyo anashikilia kushika mkono wangu asimame tusalimiane. Namwambia, ‘’Ka Mwinyi starehe, starehe…’’ Wapi hanisikii anailazimisha miguu yake isimame anisalimie mimi  mdogo wake. Mapenzi na heshima iliyoje mkubwa kumsimamia mdogo. Hivi ndivyo wazee wetu walivyotufunza. Allah awarehemu.

Kulia ni Mwinyikhamis, Abdallah Tambaza na Ibrahim wote hawa ni ndugu
wakiwa katika khitma ya Dar es Salaam Saigon Club
Niko katika, ''keyboard,'' sasa naandika. Msiba wa Chico umetugusa wengi khawa vijana wa Dar es Salaam. Mwinyikhamis alikuwa mchezaji mpira wa sifa katika New Port Club wakati wa ujana wake. Leo Mwinyi hawezi kusimama. Inanijia mechi moja ambayo naamini iko katika kumbukumbu ya wenzangu wengi wa wakti ule. New Port imepangiwa kucheza na Brazil, timu ya wababe watu wakorofi wa sifa mji mzima unawafahamu kwa shari yao ingawa walikuwa na mpira mzuri wa wachezaji wa kusifika. New Port, club ya vijana waungwana, wastaarabu wanaocheza soka la kupendeza. Mashabiki wanajiuliza itakuwaje mpira huu leo na wahuni wale? 

Saa kumi jangwani pamefurika. Hii ni mechi ya kikombe mfano wa ''league,'' kwa sasa. Wakati ule vilabu vya mtaani villikuwa na nguvu na uongozi thabiti wa kuweza kuchezesha mechi nzuri zilizojaza watazamaji na kuibua gumzo mji mzima. Brazili kuna Kitwana (Victor Mature) mbabe wa sifa, Mrisho (Wanted) mbabe wa sifa, Abdallah Mkwanda (Inger Johannsson), mbabe pia, Suleiman Jongo (Rory Calhoun) mchezaji mpole na muungwana sana lakini anacheza timu ya wababe, Mohamed Ndava. Shamte Kobe (Bingwa wa Mieleka na ngumi), Hamisi (Marlon Brando), Sadiki Ngwira (Kitonsa), Salum Hussein (Livingstone Madegwa) mtoto wa Sheikh Hussein Juma ana boli safi sana.  Wengi katika hawa wametangulia mbele ya haki Allah awarehemu. New Port wanajua kuwa leo wanacheza meshi muhimu na watu washari na wababe wa mji. 

New Port, akina Mwinyikhamis na wenzake wametandaza boli staili ya TPC mpira unatembea kwenye majani na wanakwepa hila zote za ubabe hakuna kukunjana mashati. Brazil imefedheheka kwa sababu mechi imeishia sare na wababe hawakuweza kutamba. Hata hivyo New Port wametoka kwenye mechi ile hoi kama wamepigana round 15 na Muhammad Ali. Brazil usiku ule ule wamewafata New Port club kwao kudai wapewe siku ya mechi ya marudiano. Wamefika New Port wamepanda baiskeli zao na kuziegesha kwa vishindo. Wanatafuta shari ile waliyoikosa uwanjani.

Uongozi wa New Port walifanya kikao cha haraka na uamuzi ukawa hawataki kurudiana na Brazil, wahuni wale na wapewe ushindi. Asubuhi taarifa zimeenea Kariakoo nzima na pembezoni kuwa ile mechi ya marudiano haitakuwapo New Port wamekataa kucheza na wametoa ushindi. Brazil wakautangazia mji kuwa New Port wamejisalimisha. Hii ilikuwa 1965 au 1966 maana nakumbuka mimi nilikuwa niko shule ya msingi.

Msomaji nimekuletea kisa hiki kirefu upate kujua Dar es Salaam aliyokulia Chico na sisi sote wa uzao ule ilikuwaje.

Chico alikuwa mmoja wa wacheazaji wa Everton Club iliyokuwa Mtaa wa Narung’ombe si mbali sana na nyumbani kwao Mtaa wa Tandamti mtaa aliokuwa akiishi Mzee Mshume Kiyate rafiki mkubwa wa Mwalimu Nyerere na mmoja katika wazee wa Baraza la Wazee wa TANU lililoongoza harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika. Mtaa huu umebadilishwa jina na kuitwa Mshume Kiyate lakini sasa takriban mwaka wa ishirini kibao cha jina la Mshume Kiyate hakijawekwa kwa sababu ambazi si tabu kuzifahamu. Sasa hii Everton baada ya mtafaruku ndiyo ilikuja kuundwa Saigon na baada ya muda na uhasama wa muda mfupi Everton ilikufa na wote wakajiunga na Dar es  Salaam Saigon hii tuijuayo hivi sasa. Turudi kwa Chico. 

Chico alikuwa akicheza kama mlinzi na namkumbuka Chico kwa uchezaji wake wa ukakamavu, staili ikiitwa ''kikiri,'' Chico akicheza, ''halfback,'' na alikuwa, ‘’hard tackler’’ mchezaji aliyekuwa akiingia kufata, ''loose ball,'' anakumba mpira na mguu wako. Navikumbuka viatu vyake vya mpira alivyokuwa akivaa – ''Adidas Admire.'' Kulikuwa siku zile na aina mbili za viatu vya Adidas, ''Adidas Admire,'' na ''Adidas La Plata.'' Maarufu ambavyo wengi tukivaa ilikuwa ni ''La Plata.'' Hivi vilikuwa na njumu yaani, ‘’studs,’’ unyayo mzima wakati, ''Admire,'' njumu zilikuwa chache na zilikuwa za kufunga na ‘’spanner.’’ Chico alikuwa kijana, ‘’special.’’ Simkumbuki kijana yoyote katika timu zetu za mitaani aliyekuwa akivaa, ''Admire.''

Ndani ya uwanja Chico alikuwa nahodha mzuri. Yuko nyuma na mbele marehemu Jumanne Masimenti, Jalala, Oshaka (Mazola), Mashaka (Alfredo Di Stefano), Juma Abeid, Ali Kodo, Maufi wanashambulia sauti ya Chico itasikika akihamasisha kwa Kiingereza kisafi kilichonyooka mpira upelekwe goli la adui. Utasikia akipiga kelele, ‘’Push the ball forward,’’ ‘’Score,’’ au ‘’On him,’’ yaani asiachiwe mpira adui. Inawezekana hapo anamuhimiza Ahmada Digila (Danny Blachflour) au Khalid Fadhil (George Young) wapeleke mpira mbele. Chico uongozi na ukamanda alianza toka utoto hakuanzia katika Jeshi la Polisi. Kwa kweli tulikuwa tukisikia sauti hii mori ulikuwa unapanda na hakika tukiongeza juhudi katika kushambulia au kulinda goli. Huyu Ahmada alikuwa umri wangu. Yeye ni mtoto wa Sheikh Digila wa Mtaa wa Nyamwezi nyumba yake ilikuwa karibu na msikiti wa Makonde. Ahmada alipata elimu kubwa sana ya dini. Ahmada alikuwa na kasi ya ajabu katika kusoma Qur’an. Kwenye khitma yeye anawea kukumalizia juzuu hata tatu wewe moja hujakamilisha. Alikuwa ''midfielder,'' hodari katika vijana wa Saigon pamoja na Hassan (Gilbert Mahinya). Hassan Gilbert baadae alikuwa kuwa mtaalamu wa, ''Systems,'' katika moja ya mashirika ya umma na siku tulipokutana Mlimani City akiwa na mabinti zake wakubwa waliojipamba kwa hijab alinifahamisha kuwa amestaafu kazi baada ya kufikisha miaka 60. Nilpomfahamisha kuwa nami nami pia nishapumzika akanambia taarifa zangu anazo kwani alikuwa akinifuatilia huko Tanga nilipokuwa nafanyakazi. Nilifarajika kusikia hayo kuwa hata baada ya miaka ya kutengana wana Saigon walikuwa wakitaka kujua nani yuko wapi na anafanya nini.

Hivi ninavyoandika ni kama vile najiona niko Mnazi Mmoja tunafanya mazoezi na wakati mwingine tukijifunza kuachiana pasi za haraka za kuwazuga maadui. Namuona Ghalib Hamza, maarufu kwa jina la Guy. Chico juu ya ushujaa wake wa kuwakumba washambuliaji hathubutu kumfata Guy akiwa na mpira. Guy alikuwa hana kimo, mfupi lakini ana maungo kiasi. Kilichokuwa kikitutisha kwa Guy ni ile, ‘’ball control,’’ yake na ‘’dribbling skills,’’ angeweza kumzunguka Chico na hata kumtia harusi, yaani kupitisha mpira katikati ya miguu yake. Kulikuwa na Mohamed Ramadhani Kondo (Garincha), Rashid Vava mchezaji rafu club nzima tukimuogopa.  Wote wenzetu hawa wametangulia mbele ya haki. Naamini wasomaji vijana watapata tabu sana kuelewa haya majina niliyoyataja, hizi ''nicknames za akina Mazola, Di Stefano, Blanchflour. Hawa walikuwa katika wakati wetu wa miaka ya 1960 ndiyo wachezaji mpira maarufu wa vilabu tofauti vya Ulaya.

Chico alikuwa na baiskeli yake, ‘’sports’’ nyuma aliiandika, ‘’Thunderbird’’ na mwenyewe akiita baiskeli yake kwa jina hilo. Alikuwa anaipanda kwenda shule kavaa vizuri sana na kichwani kavaa, ‘’baseball cap.’’ Amechomekea shati lake jeupe alilolivalia T Shirt nyeupe ndani ndani na kiunoni amevaa, ‘’army belt.’’ Hii ilikuwa mikanda myeupe ya ‘’canvass,’’ yenye, ''buckle,'' ya fedha  au ''gold,'' inayong’aa. Mmarekani amekwishakazi. Vijana wote tuliokuwa tukijiona, ‘’fashionable,’’ tukivaa hivyo lakini Chico mwenzetu alitushinda kwa kuwa ilikuwa kama vile mambo yale yako katika damu yake. 

Nakikumbuka vyema chumba chake pale kwao. Kilikuwa nadhifu na alikuwa na ‘’record player,’’ yake na sahani za santuri nyingi za nyimbo mbalimbali za wanamuziki wa zama zile. Sasa hapo ndipo utakapotambua kuwa Chico alikuwa, ‘’special.’’ Mimi nilikuwa na ‘’record player,’’ yangu, ‘’Dansette,’’ imetengenezwa Uingereza, Sussex, nakumbuka ile label. Chico santuri zake zilikuwa ni Nat King Cole, Ray Charles, Dean Martin na wanamuziki mfano wa hao kama Sammy Davis na wengine. Muziki mgeni kwa wengi kwa wakati ule. Nyimbo alizokuwa akizipenda na akaniambukiza na mimi kuzipenda ni, ‘’Ramblin Rose,’’ na ‘’The Good Times,’’  zote za Nat King Cole. Hadi leo kila nikizisikia nyimbo hizi huwa nakumbuka utoto wetu katika mitaa ya Kariakoo.



Kushoto mstari wa mbele Hussein Shebe, Henin Seif, kulia wa pili ni Raymond Chihota, Hussein,
(pass) Mbaraka ''Bata'' picha ilipigwa mapema 1960

Miaka ya 1960 ilikuwa miaka ya patashika si Dar es Salaam tu bali dunia nzima na ndiyo maana Waingereza wakaipa jina miaka hiyo kuwa ni, ‘’Roaring 60s.’’ Dar es Salaam ilikuwa na mastaa wake wakivuma kama Hussein Shebe, Raymond Chihota na Henin Seif kuwataja wachache  katika Chipukizi Club, timu ya waimbaji vijana wakipigiwa muziki na The Blue Diamonds,  ''band,'' ya vikana wa Kigoa. Kulikuwa na Sammy Davis Jr Salim Hirizi akiimba nyimbo maarufu, ''Summer Time,'' kwa umahiri mkubwa.  Katika hawa waimbaji kubwa lao alikuwa Sal Davis. Siku Sal Davis alipokuja na Hussein Shebe Mtaa wa Tandamti kuwaamkia wazee wake Hussein nyumbani kwa kina Mohamed Jaggan ilikuwa gumzo la mtaa mzima na sisi ambao hatukuwapo kumuona Sal Davis tulisikitika sana. Uhuru wa Tanganyika uliingiza katika nchi mambo mengi kutoka Ulaya yaliyotuvutia sisi vijana. Huu ulikuwa wakati wa wazimu wa mambo mengi sana kutoka Marekani na Ulaya. Sote tukisukumwa na ujana tulikumbwa na wimbi hili. Haya ndiyo yalikuwa maisha ya sisi vijana katika Dar es Salaam ya miaka ile ya 1960 na Chico hakuweza kuliepuka wimbi hili kama vijana wengi walivyoshindwa.


Salum ''Sammy Davis Jr'' Hirizi kama alivyo hivi sasa

Sal Davis Katika Onyesho Ujerumani 1960s

Ilikuwa Chico ndiyo, ‘’alinijulisha,’’ mimi kwa Sidney Poitier na nikaanza kuingia kila senema yake ilipokuja mjini. Sidney Poitier katika miaka ile hakuwa maarufu kwa vijana wengi wa Dar es Salaam. Wengi wetu tulikuwa na John Wayne, Richard Widmark, Alan Ladd, Victor Mature, Marlon Brando na mfano wa hao na wala haikutupitikia kuwa tunaweza kwenda senema Empire, Avalon, Empress au Chox kuangalia senema, ‘’actor,’’ Mnegro kama Sidney Poitier au Jim Brown. Chico alikuwa, ‘’special,’’ yeye akimjua Sidney Poitier, Eartha Kitt na wengineo siku nyingi sana. Kuanzia hapo na mimi nikabadilika. Nakumbuka senema za Sidney Poitier alizokuwa akipenda kunihadithia kama ni kama ''Lilies of the Fied,’’ ‘’A Patch of Blue,’’ na nyingine nyingi.

Image result


Ujana haukawii kukimbia. Haukupita muda tukakua na ikawa lazima tukubali kuwa wakati wa mchezo umepita tunaingia ukubwani. Chico alitushangaza wengi alipojiunga na Jeshi la Polisi kwani si katika kazi ambazo, ‘’watoto wa mjini,’’ tulizipenda na kubwa ni kuwa kazi ya jeshi ilikuwa inahitaji kufanyakazi nje ya Dar es Salaam na wengi wakiona dhiki kuondoka mjini. Sasa hapa ndipo ninapotaka kuhitimisha kuwa Chico alikuwa, kwa kweli na kwa hakika kabisa alikuwa ‘’special.’’ 

Chico alijiunga na Jeshi la Polisi na aliitumikia nchi yake kwa uadilifu mkubwa. Alifanyakazi takriban kila mahali na kuacha jina lililotukuka. MIaka mingi baada ya sisi kutoweka hapa duniani, itakapokujaandikwa historia ya watoto wa Dar es Salaam na nini wamefanya katika taifa hili nina hakika Kamanda Chico jina lake litakuwa juu. 

Allah amlaze pema ndugu yetu Mohamed Awadh Saiwaad maarufu kwa jina la Chico aliloishi nalo utotoni hadi ukubwani. 

Mwandishi akiwa Viwanja Vya Mnazi Mmoja ambako Everton na kisha Saigon
walikokuwa wakicheza mpira. Nyuma ni barabara iliykuja kupewa jina la Bi. Titi 
Mohamed na ukivuka barabara hiyo ni Soko la Kisutu maarufu kwa jina la Soko 
Mjinga. Picha ilipigwa 1966

Friday, 2 December 2016

Kushoto mbele: Hussein Shebe. Henin Seif, Raymand Chihota
Nyuma ya Hussein ni Mbaraka
Hussein Shebe wa pili kushoto na Ashantis

Kulia Henin Seif, Hussein Shebe, Nassor na Mohamed Said



Bukyanagandi,
Mzee Chihota 
alikuwa Meneja wa Arnatouglo Hall nadhani alipotoka yeye
ndiye akaja Denis Phombeah, Mnyasa.

Mzee Chihota alikwenda masomoni Uingereza na huko mauti yakamfika na

alizikwa huko huko.

Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1950s.
Kuna Mtaa Temeke umepewa jina, ''Chihota,'' kwa heshima yake. 

Kulikuwa na Norman Chihota bingwa wa 100 metres na Raymond kaka
yake.

Hawa walitoka Rhodesia.


Gershom Chihota nilisomanae St. Joseph's School na tukicheza mpira sote

na kupiga muziki yeye akipiga bass guitar.

Gershom Chihota
Baada ya uhuru kupatikana walirudi kwao na huko Raymond alifariki.
Huyu alisoma Urusi na alioa Mrusi.

Raymond alipomaliza shule Aga Khan alifanyakazi TBC kama mtangazaji na

allikuwa na kipindi, ''Teenagers Time,'' akipiga pop music akina Cliff Richard,
Helen Shapiro, Elvis Presly, Beatles, Rolling Stones etc.

Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa mmoja wa ''Chipukizi,'' na akina Henin
Seif, Abdul Nanji, Badrin,
 Salum Hirizi (Sammy Davis), Yusuf Ramia, Hussein Shebe, Cuthbert Sabuni,
Sauda Mohamed, Maryam Zialor
 na vijana wengi wa Dar es Salaam.

Ray alikuwa mwimbaji mzuri wa nyimbo za Kizungu na Chipukizi na yeye kwa
msaada wa David Wakati wakaanzisha kipindi RTD, ''Chipukizi Club.''

Kipindi hiki kilipendwa sana na vijana hadi pale kilipokuja kupigwa marufuku na

Regiional Commissioner wa Dar es Salaam, Mustafa Songambele kwa sabau ati
kinatukuza utamaduni wa kigeni.


Mustafa Songambele

Songambele hakupendezewa na zile nyimbo za Kizungu bendi ile ya Chipukizi
walizokuwa wakipiga.

Chipukizi walikuwa wakipiga pamoja na vijana wa Kigoa wakijiita, ''The Blue Diamonds.''

Walikuwa na wapiga magitaa hodari sana.

Hii ilikuwa 1963/64.


Ray
na Yusuf Baruti wakaenda kusoma Urusi na ''members,'' wengi wa Chipukizi wakaondoka kwenda
nje.

Hussein Shebe akaenda Nairobi kujiunga na Ashantis kama muimbaji na kwa kweli

aliipaisha ile bendi na hawakukaa sana Nairobi wakenda Addis Ababa wakawa
wanapiga Wabe Shebelle Hotel, hotel kubwa sana wakati ule.

Sal Davis ndiye aliyemchukua Hussein kumpeleka Nairobi.


Sal alikuja Dar es Salaam na alifanya show moja na Chipukizi Radio Tanzania na hapo

ndipo alipomsikia Hussein akiimba.


Sal Davis na Meneja wa Philips Uwanja wa Ndege Nairobi aliporudi na nyimbo ya kumsifia
Jomo Kenyatta wakati wa uhuru 1963

Badrin na Nanji wao walikwenda America.


Sabuni na bendi yake, ''The Flaming Stars,'' akiwa na Peter Kondowe (Peco) na

George Mzinga wao wakaenda Mombasa.

Miaka mingi baadae nilifika Addis Ababa na nilikaa Wabe Shebelle lakini hoteli ilikuwa

taaban, imechoka.

Nakumbuka nililetewa Coke lakini sikuweza kuitambua chupa jinsi ilivyokuwa imesagika.


Hii ilikuwa 1989 enzi ya Mengitsu Haile Mariam na Hussein Shebe na Ashanti

wamekimbia wanapiga muziki wao Italy.

Nakumbuka Ray aliporudi alikaribishwa Radio Tanzania English Service kwa mahojiano

katika kipindi cha muziki.

katika nyimbo alizochagua apigiwe moja naikumbuka kwa kuwa nami nikiipenda,

''Let The Good Times Roll,'' ya Ray Charles.

Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom na Norman na bahati

nzuri nilikutananao.

Nina picha nikizipata nitaziweka hapa In Shaallah.


Baada ya miaka mingi sana nilikutana na Hussein Shebe kwenye boat tunakuja Dar es

Salaam kutoka Zanzibar nilikuwa na rafiki yangu Tamim Faraj.

Tulikumbusha mengi na akanipa cassette yake na Ashanti.


Hivi sasa Hussein amepumzika muziki na akiwa na nafasi hupita nyumbani kwangu

kunijulia hali kila anapokuja kutoka Zurich anakoishi na mkewe Mswiss na wanae na kila
siku ananikaribisha Switzerland.

Ingia You Tube ustaladhi na muziki wa Hussein Shebe.


Katika mahojiano nliyofanya na Hussein ananambia kuwa siku alipomwabia Meneja wake

kuwa yeye muziki basi alishtuka na akambembeleza sana.

Hussein hajatazama nyuma.

Mke wake anasema, ''Huyu Hussein toka amerudi kwenye Uislam wake...''

Siku moja nafanya mahojiano na Hussein.

Ghafla ananyanyuka ananambia, ''Mohamed Maghrib sasa tuswali kwanza...''

Machozi yalinilengalenga...

Tulikuwa nyumbani kwa rafiki yake toka udogo wao - Henin Seif.

Kakutana na mke wangu msikitini anamwambia, ''Mohamed si rafiki yangu ni ndugu yangu...''

When the great American trumpeter and singer, Louis Armstrong, visited Kenya in 1960, he expressed his admiration for a nine-year-old guitarist from Kaloleni Estate, Nairobi.

The young boy who had played a few tracks for Armstrong at a private function was Paddy Gwada and the legendary jazzman was so overwhelmed by this prodigious talent that, it is said, he even offered to adopt him.

Born in Mombasa, Paddy and his brother, Rocky, who plays the saxophone, were the leaders of the Bata Shoeshine Boys, a band promoted by impresario, Peter Colmore.
The group was sponsored by the famous Bata Shoe Company and they became television stars in Kenya through their performances on the Bata Shoe Box game show in the early 1960s.

Their most popular recording is a song that many people are familiar with, but may not associate with the group. Africa Sunset, recorded by the Shoeshine Boys in 1965, is perhaps better known as the instrumental signature tune to the television courtroom comedy, Vioja Mahakamani.

After the end of their contract with Bata, the group changed its name to The Ashantis and in 1966, became the resident band at the Starlight Club in Nairobi. Two years later, Sal Davis arranged a performance stint for them in Addis Ababa, Ethiopia.

From Addis, the Ashantis left for Denmark in 1971, before eventually settling in Switzerland, where the band remains to this day. In the picture above, band member Hussein Shebe (right) with emperor Haile Selassie. (Daily Nation 12 August 2013)

Saturday, 24 September 2016



Vijana wa Chipukizi
Chipukizi Club





















Bukyanagandi,
Mzee Chihota 
alikuwa Meneja wa Arnatouglo Hall nadhani alipotoka yeye
ndiye akaja Denis Phombeah, Mnyasa.

Mzee Chihota alikwenda masomoni Uingereza na huko mauti yakamfika na
alizikwa huko huko.

Hii ilikuwa miaka ya mwanzoni 1950s.
Kuna Mtaa Temeke umepewa jina, ''Chihota,'' kwa heshima yake. 

Kulikuwa na Norman Chihota bingwa wa 100 metres na Raymond kaka
yake.

Hawa walitoka Rhodesia.

Gershom Chihota nilisomanae St. Joseph's School na tukicheza mpira sote
na kupiga muziki yeye akipiga bass guitar.

Baada ya uhuru kupatikana walirudi kwao na huko Raymond alifariki.
Huyu alisoma Urusi na alioa Mrusi.

Raymond alipomaliza shule Aga Khan alifanyakazi TBC kama mtangazaji na
allikuwa na kipindi, ''Teenagers Time,'' akipiga pop music akina Cliff Richard,
Helen Shapiro, Elvis Presly, Beatles, Rolling Stones etc.

Ray kama alivyokuwa akijulikana alikuwa mmoja wa ''Chipukizi,'' na akina Henin
Seif, Abdul Nanji, Badrin,
 Salum Hirizi (Sammy Davis), Yusuf Ramia, Hussein Shebe, Cuthbert Sabuni,
Sauda Mohamed, Maryam Zialor
 na vijana wengi wa Dar es Salaam.



Photo: SALIM HARIZ
Salum Hirizi (Sammy Davis) 2016
Kushoto ni Abdul Nanji kama alivyo hivi sasa n na John Mtembezi
Ray alikuwa mwimbaji mzuri wa nyimbo za Kizungu na Chipukizi na yeye kwa
msaada wa David Wakati wakaanzisha kipindi RTD, ''Chipukizi Club.''

Kipindi hiki kilipendwa sana na vijana hadi pale kilipokuja kupigwa marufuku na
Regiional Commissioner wa Dar es Salaam, Mustafa Songambele kwa sabau ati
kinatukuza utamaduni wa kigeni.


Mustafa Songambele 2015
Songambele hakupendezewa na zile nyimbo za Kizungu bendi ile ya Chipukizi
walizokuwa wakipiga.

Chipukizi walikuwa wakipiga pamoja na vijana wa Kigoa wakijiita, ''The Blue Diamonds.''
Walikuwa na wapiga magitaa hodari sana.

Hii ilikuwa 1963/64.

Ray
na Yusuf Baruti wakaenda kusoma Urusi na ''members,'' wengi wa Chipukizi wakaondoka kwenda
nje.

Hussein Shebe akaenda Nairobi kujiunga na Ashantis kama muimbaji na kwa kweli
aliipaisha ile bendi na hawakukaa sana Nairobi wakenda Addis Ababa wakawa
wanapiga Wabe Shebelle Hotel, hotel kubwa sana wakati ule.

Sal Davis ndiye aliyemchukua Hussein kumpeleka Nairobi.

Sal alikuja Dar es Salaam na alifanya show moja na Chipukizi Radio Tanzania na hapo
ndipo alipomsikia Hussein akiimba.


Sal Davis na Meneja wa Philips Uwanja wa Ndege Nairobi aliporudi na nyimbo ya kumsifia
Jomo Kenyatta wakati wa uhuru 1963


Badrin na Nanji wao walikwenda America.

Salum Hiirizi anasema nyimbo ambayo Badrin akipenda kuimba ilikuwa, ''Fame
and Fortune,'' ya Elvis Presley

Sabuni na bendi yake, ''The Flaming Stars,'' akiwa na Peter Kondowe (Peco) na
George Mzinga wao wakaenda Mombasa.

Miaka mingi baadae nilifika Addis Ababa na nilikaa Wabe Shebelle lakini hoteli ilikuwa
taaban, imechoka.

Nakumbuka nililetewa Coke lakini sikuweza kuitambua chupa jinsi ilivyokuwa imesagika.

Hii ilikuwa 1989 enzi ya Mengitsu Haile Mariam na Hussein Shebe na Ashanti
wamekimbia wanapiga muziki wao Italy.

Nakumbuka Ray aliporudi alikaribishwa Radio Tanzania English Service kwa mahojiano
katika kipindi cha muziki.

katika nyimbo alizochagua apigiwe moja naikumbuka kwa kuwa nami nikiipenda,
''Let The Good Times Roll,'' ya Ray Charles.

Mwaka wa 1993 nilikwenda Harare na nilimtafuta Gershom na Norman na bahati
nzuri nilikutananao.

Nina picha nikizipata nitaziweka hapa In Shaallah.

Baada ya miaka mingi sana nilikutana na Hussein Shebe kwenye boat tunakuja Dar es
Salaam kutoka Zanzibar nilikuwa na rafiki yangu Tamim Faraj.

Tulikumbushana mengi na akanipa cassette yake na Ashanti.

Hivi sasa Hussein amepumzika muziki na akiwa na nafasi hupita nyumbani kwangu
kunijulia hali kila anapokuja kutoka Zurich anakoishi na mkewe Mswiss na wanae na kila
siku ananikaribisha Switzerland.

Ingia You Tube ustaladhi na muziki wa Hussein Shebe.

Katika mahojiano nliyofanya na Hussein ananambia kuwa siku alipomwambia Meneja wake
kuwa yeye muziki basi alishtuka na akambembeleza sana.

Hussein hajatazama nyuma.
Mke wake anasema, ''Huyu Hussein toka amerudi kwenye Uislam wake...''

Siku moja nafanya mahojiano na Hussein.
Ghafla ananyanyuka ananambia, ''Mohamed Maghrib sasa tuswali kwanza...''

Machozi yalinilengalenga...
Tulikuwa nyumbani kwa rafiki yake toka udogo wao - Henin Seif.

Kakutana na mke wangu msikitini anamwambia, ''Mohamed si rafiki yangu ni ndugu yangu...''



Kulia Raymond Chihota, Henin Seif, Hussein Shebe
Nyuma ya Hussein Shebe Mbaraka Bata, Nyuma ya Henin Seif Hussein

Photo: HUSSEN SHEBE, HENIN SEIF, NASSER AND ME
Kulia: Henin Seif, Hussein Shebe, Nasser na Mwandishi 2013


Photo:
Kulia: Henin Seif, Hussein Shebe na Nasser

Saturday, 4 June 2016


Muhammad Ali 1942 – 2016

Photo

Muhammad Ali alipata kusema baada yangu mimi kutakuwa hakuna tena ngumi. Hivi ndivyo ilivyo. Si watu wengi baada ya Ali kuondoka ulingoni waliendelea kufuatilia tena ngumi. Ali alichukua ubingwa kwa kumpiga Sony Liston mwaka wa 1964 wakati ule aikijulikana kama Cassius Clay. Miaka ya 1960 imepewa jina la ‘’The Roaring 60s’’ kwa sababu ilikuwa miaka ya mengi sana. Huu ulikuwa wakati ambao sisi ambao sasa ni watu wazima au ukipenda ni wazee tulikuwa vijana katika miaka ya ‘’teens’’ – ‘’teenegers.’’ Ilikuwa ndiyo miaka ya Muhammad Ali na Sony Liston, ilikuwa miaka ya Sam Cooke, Beatles na Rolling Stones, ilikuwa miaka ya Eric Bardon na Animals…ilikuwa miaka ya Martin Luther King. Elvis Presley na Cliff Richard. Ilikuwa miaka ya Woodstock. Miaka ya Jimi Hendrinx na Janis Joplin. Hapa kwetu East Africa tulikuwa na nyota yetu - Sal Davis na ''Makini'' nyimbo yake iliyovuma aliyoitoa mwaka wa 1963. Dar es Salaam tulikuwa na Chipukizi Club na Hussein Shebe. Henin Seif na Raymond Chihota wakitumbuza na band ya vijana wa Kigoa ikiitwa The Blue Diamonds. 

Ilikuwa miaka ya wazimu kwa hakika ilikuwa miaka ya wazimu khasa. Vita vya Vietnam vilikuwa vinaendelea kila ukifungua radio habari ni za Saigon na Hanoi. Huu ndiyo wakati yalipotokea mauaji ya kutisha ya Mai Lai huko Vietnam. Juu ya vurugu hizi zote aliyekuwa aking’ara na ‘’icon,’’ ya wengi alikuwa Muhammad Ali Bingwa wa Dunia wa Masumbwi wa Uzito wa Juu. Hodari wa kuzungumza wakati mwingine kwa mashairi: ‘’Harry Cooper has been talking too much, he will go down in five.’’ ‘’Fly like a butterfly and sting like a bee. Rumble young man rumble.’’ 

Ali akiburudisha ndani na nje ya ulingo. Ni tabu kwa mtu kujaribu kumweleza Muhammad Ali kwani kaandikwa sana tena na waandishiwa kutajika. Nataka kumalizia kwa kusema kuwa moja ya vitabu vyangu katika orodha ya vitabu ninavyovipenda na hurudia kuvisoma tena na tena na tena kila nipatapo nafasi ni kitabu alichoandika mwenyewe Ali kuhusu maisha yake: ‘’The Greatest My Own Story.’’

Miaka miwili iliyopita niliandika maneno haya katika JF:




Hoolligan,
Nataka nikupe habari za Ali.

Nikimpenda toka udogo wangu nina miaka 12 mwaka 1964 Ali alipochukua
mkanda.

Nilifika Guy Madison Square Garden New York pale imewekwa picha kubwa
sana ya Ali na Joe Frazier.

Nilisimama kuitazama ile picha kwa muda mrefu sana na ikanikumbusha mengi.

Kwanza ikiwa hujasoma kitabu chake kitafute, ''The Greatest My Own Story.''

Ali alipompiga Sonny Liston 1964 wengi walimsifia Ali siku hizo akiitwa Cassius Clay.

1974 alipokuwa anajitayarisha kupigana na George Foreman mtu wake wa massage
Mzee kutoka Cuba alimwambia kuwa Sonny Liston hakuwa chochote.

Ikiwa Ali kwa hakika anataka adhihirishe kuwa yeye ni ''Greatest,'' basi ampige Foreman.

Yule mzee kutoka Cuba alimfananisha Forema na simba na Ali mtu anaetaka kuingia
katika tundu lake kuchukua nyama.

Foreman alikuwa yeye akifika round ya tatu mpinzani anakuwa keshalala chini flat.

Walipomaliza round ya pili sasa wanakwenda ya tatu wapambe wa Foreman wakawa
wanamwambia Foreman kwa sauti ya juu, ''Finish him off.''

Akiwa katika kigoda chake kwenye corner yake daktari wake Dk. Pacheco akamwambia
Ali, ''Unasikia jamaa wanavyosema?''

Ali akajibu, '' Huyu mimi nampiga.''
Pacheco akashangaa akamwambia Ali,'' Basi mpige tumalize hili pambano.''

Ali akamwambia Dk. Pacheco,''Let us have some fun first.''

The rest is history.

Attached Files: