Monday, 15 December 2014

UTUNUKU WA NISHANI KWA WAISLAM WALIOCHANGIA KATIKA MAENDELEO YA UISLAM TANZANIA


Katika mkutano wa mwaka uliofanyika Pongwe, Tanga Jukwaa la Vijana wa Kiislam waliwatunuku Waislam waliochangia katika maendeleo ya Uislam Tanzania katika nyanja tofauti. Jukwaa limeazimia kutoa nishani kila mwaka kuwaenzi wote ambao wameacha alama katika historia ya Uislam nchini. Mwaka huu Jukwaa lilitoa nishani kwa hawa wafuatao:
  1. Sheikh Hassan bin Amir
  2. Sheikh Mohammed Ayub
  3. Prof. Kighoma Ali Malima
  4. Sheikh Mselem bin Ali
  5. Sheikh Ponda Issa Ponda
  6. Burhan Mtengwa
  7. Mussa Mdidi
  8. Mohamed Kasim
  9. Omari Msangi
  10. Ilunga Hassan Kapungu
  11. Arif Nahdi
  12. Dk. Khalid A. Abdullah
  13. Jaffari Siraji
  14. Abdallah Mtaki
  15. Mohamed Said
Mwandishi aliombwa aeleze historia fupi za waliotunukiwa na yeye alifanya hivyo kwa wale aliokuwa akifahamu historia zao kama vile Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Mohamed Ayub, Prof. Kighoma Malima, Sheikh Ponda Issa Ponda, Burhan Mtengwa, Mussa Mdidi, Mohamed Kassim, Omari Msangi na Ilunga Hassan Kapungu na hao waliobakia historia zao zilielezwa na watu wengine mmojawapo akiwa Sheikh Shemtoi ambae alieleza historia ya Sheikh Mselem bin Ali na ya Dk. Khalid Abdullah.

Hamisi Sindato Naibu Katibu Mkuu wa Jukwaa la Vijana wa Kiislam Tanzania
Akizungumza Kabla ya Utunuku wa Nishani

Wajumbe wa Mkutano wa Jukwaa la Vijana wa Kiislam Tanzania
Zein Abdallah Ayub Mtoto wa Sheikh Abdallah Ayub Mdogo wa Sheikh Mohamed Ayub
 Akipokea Nishani ya Marehemu Sheikh Mohamed Ayub


Kijana Kutoka Zanzibar Suleiman Ally Said Akipokea Nishani ya 
Sheikh Hassan bin Amir kwa Niaba ya Watoto na Wajukuu wa 
Sheikh Hassan bin Amir na kwa Niaba ya Watu wa Zanzibar


Shaib Ally Mselem Akipokea Nishani kwa Niaba ya Baba Yake 
Sheikh Mselem bin Ally Ambae Yuko Mahabusi Akikabiliwa na Kesi ya Ugaidi


Al Marhum Sheikh Mohamed Ayub Muasisi wa Shamsiyya Tanga
Hapa anaonekana Akisomesha Tafsir ya Qur'an

Arif Nahdi (Katikati) Alipotunukiwa Nishani Katika Ramadhani Conference Mwaka 2013
Sheikh Mselem bin Ali na Mwandishi Picha Imepigwa Mwaka 2012 Kwenye
Madras ya Sheikh Mselem, Zanzibar 

Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Hivi Sasa Yuko Rumande
Akikabiliwa na Kesi Mbili


Marehemu Jaffar Siraji Kulia Aliyevaa Kanzu ya Grey


Ustadh Jamal Mangale Akipokea Nishani ya Mwalimu Wake Marehemu Jaffar Siraji

Ahmada Ayub Mwenyekiti Taifa wa Jukwaa la Vijana
Mwandishi Akipokea Nishani Yake Kutoka kwa Mwenyekiti Taifa Jukwaa la
Vijana wa Kiislam Tanzania Ahmada Ayub

Marehemu Sheikh Ilunga (Mstari wa Mwisho Kulia Mwisho) Wakati wa Ujana Wake
Mstari wa Mwanzo wa Pili Kutoka Kulia ni Mwandishi
Picha Hii Ilipigwa Mwaka 1988 Dodoma Chuo Cha Biashara Katika
Semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania


2 comments:

Mohamed Said Historia, Siasa na Maendeleo Tanzania said...

Utunuku wa Nishani kwa Waislam Walio Hai na Waliotangulia...

Unknown said...

Salaam aleykum my brother Mohamed Said,ninafarajika sana kila nikitembelea blog yako,wewe ni mhistoria mzuri sana hapa Tanzania hivi sasa na hakuna yeyote yule anayeweza kuandika historia iliyofanywa na wazee wetu wa kiislam bara na hata visiwani,unanitia moyo kila nitembeleapo blog yako ,kama vile shahidi brother Ilunga alivyofanya(adhabu za kuburi zimuondokee)