Katika mkutano wa mwaka uliofanyika Pongwe, Tanga Jukwaa la Vijana wa Kiislam waliwatunuku Waislam waliochangia katika maendeleo ya Uislam Tanzania katika nyanja tofauti. Jukwaa limeazimia kutoa nishani kila mwaka kuwaenzi wote ambao wameacha alama katika historia ya Uislam nchini. Mwaka huu Jukwaa lilitoa nishani kwa hawa wafuatao:
- Sheikh Hassan bin Amir
- Sheikh Mohammed Ayub
- Prof. Kighoma Ali Malima
- Sheikh Mselem bin Ali
- Sheikh Ponda Issa Ponda
- Burhan Mtengwa
- Mussa Mdidi
- Mohamed Kasim
- Omari Msangi
- Ilunga Hassan Kapungu
- Arif Nahdi
- Dk. Khalid A. Abdullah
- Jaffari Siraji
- Abdallah Mtaki
- Mohamed Said
Mwandishi aliombwa aeleze historia fupi za waliotunukiwa na yeye alifanya hivyo kwa wale aliokuwa akifahamu historia zao kama vile Sheikh Hassan bin Amir, Sheikh Mohamed Ayub, Prof. Kighoma Malima, Sheikh Ponda Issa Ponda, Burhan Mtengwa, Mussa Mdidi, Mohamed Kassim, Omari Msangi na Ilunga Hassan Kapungu na hao waliobakia historia zao zilielezwa na watu wengine mmojawapo akiwa Sheikh Shemtoi ambae alieleza historia ya Sheikh Mselem bin Ali na ya Dk. Khalid Abdullah.
Hamisi Sindato Naibu Katibu Mkuu wa Jukwaa la Vijana wa Kiislam Tanzania Akizungumza Kabla ya Utunuku wa Nishani |
![]() |
Wajumbe wa Mkutano wa Jukwaa la Vijana wa Kiislam Tanzania |
Zein Abdallah Ayub Mtoto wa Sheikh Abdallah Ayub Mdogo wa Sheikh Mohamed Ayub Akipokea Nishani ya Marehemu Sheikh Mohamed Ayub |
Kijana Kutoka Zanzibar Suleiman Ally Said Akipokea Nishani ya Sheikh Hassan bin Amir kwa Niaba ya Watoto na Wajukuu wa Sheikh Hassan bin Amir na kwa Niaba ya Watu wa Zanzibar Shaib Ally Mselem Akipokea Nishani kwa Niaba ya Baba Yake Sheikh Mselem bin Ally Ambae Yuko Mahabusi Akikabiliwa na Kesi ya Ugaidi |
|
Al Marhum Sheikh Mohamed Ayub Muasisi wa Shamsiyya Tanga Hapa anaonekana Akisomesha Tafsir ya Qur'an |
![]() |
Arif Nahdi (Katikati) Alipotunukiwa Nishani Katika Ramadhani Conference Mwaka 2013 |
Sheikh Mselem bin Ali na Mwandishi Picha Imepigwa Mwaka 2012 Kwenye Madras ya Sheikh Mselem, Zanzibar |
![]() |
Sheikh Ponda Issa Ponda Katibu wa Baraza Kuu la Waislam Hivi Sasa Yuko Rumande Akikabiliwa na Kesi Mbili |
Marehemu Jaffar Siraji Kulia Aliyevaa Kanzu ya Grey Ustadh Jamal Mangale Akipokea Nishani ya Mwalimu Wake Marehemu Jaffar Siraji |
Ahmada Ayub Mwenyekiti Taifa wa Jukwaa la Vijana |
![]() |
Mwandishi Akipokea Nishani Yake Kutoka kwa Mwenyekiti Taifa Jukwaa la Vijana wa Kiislam Tanzania Ahmada Ayub |
![]() |
Marehemu Sheikh Ilunga (Mstari wa Mwisho Kulia Mwisho) Wakati wa Ujana Wake Mstari wa Mwanzo wa Pili Kutoka Kulia ni Mwandishi Picha Hii Ilipigwa Mwaka 1988 Dodoma Chuo Cha Biashara Katika Semina ya Vijana wa Kiislam Tanzania |
2 comments:
Utunuku wa Nishani kwa Waislam Walio Hai na Waliotangulia...
Salaam aleykum my brother Mohamed Said,ninafarajika sana kila nikitembelea blog yako,wewe ni mhistoria mzuri sana hapa Tanzania hivi sasa na hakuna yeyote yule anayeweza kuandika historia iliyofanywa na wazee wetu wa kiislam bara na hata visiwani,unanitia moyo kila nitembeleapo blog yako ,kama vile shahidi brother Ilunga alivyofanya(adhabu za kuburi zimuondokee)
Post a Comment